KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, October 16, 2013

Mabondia waafrika walemewa Kazakhstan Selemani Kidunda atacheza Mandeep Jangra wa India hii leo.

Bondia selemani Kidunda kulia naye anashiriki
Mashindano ya ndondi ya ubingwa wa dunia yanazidi kupamba moto mjini Almaty, Kazakhstan.
Kufikia sasa ni mabondia wawili tu wa Afrika, Efetobor Apochi wa Nigeria uzani wa heavy na Colin Louis wa Mauritius ambao wameshinda mapigano yao na wengine sita kutoka Kenya, Misri, Angola na Nigeria wakashindwa.
Efetobor alimshinda kwa pointi Seyda Keser wa Uturuki naye Louis akamchapa kwa pointi pia Khatuev Salavat wa Norway.
Mabondia sita walioshindwa ni Dan Shisia uzani wa heavy, John Kariuki uzani wa light na Dennis Okoth uzani wa light-welter wote wa Kenya, Vivaldo Rodrigues wa Angola uzani wa fly, Olayinka Yusuff wa Nigeria uzani wa fly na Mohammed Eslam wa Misri uzani wa light-welter aliyeshindwa na Yves Ulysse wa Canada.
Shisia alichapwa na Jim Andreasen wa Denmark kwa pointi, Kariuki akashindwa na Dorjnyambuu Otgondalai wa Mongolia.
Bondia huyo wa Kenya alipata jeraha juu ya jicho lake la kulia hivyo basi refarii akaamua hawezi kuendelea.
Mashabiki wa ndondi mjini Almaty waliachwa vinywa wazi wakishangaa vile bondia wa Uturuki Fatih Keles alivyomshinda Okoth kwa pointi 2-1.
Makocha wa Kenya Albert Matito na George ''Foreman’’ Onyango wanasema mashabiki waliwazomea majaji kwa uamuzi huo wakisema bondia wa Kenya alistahili kushinda kwa sababu alimlemea mwenzake raundi zote.
Vivaldo Rodrigues wa Angola alishindwa kwa pointi na Malik Jackson wa Marekani uzani wa fly, na bondia mwingine wa Nigeria Olayinka Yusuf akashindwa na Charlie Edwards wa England uzani wa fly.
Jumatano wiki hii Raytoin Okwiri wa Kenya na Selemani Kidunda wa Tanzania, wote uzani wa welter, wataingia ulingoni kwa mapigano yao ya kwanza. Okwiri anazipiga na Daniel Lewis wa Australia huku Kidunda akipambana na Mandeep Jangra wa India…

No comments:

Post a Comment