Zambia imetoa vibali vya kukamatwa kwa wachezaji wake
watatu waliokosa mechi ya kirafiki dhidi ya Brazil mjini Beijing China.
Hata hivyo Zambia ilishindwa na Brazil mabao mawili kwa nunge.
Klabu ya DRC TP Mazembe ilisisitiza kuwa
wachezaji hao Rainford Kalaba, Stoppila Sunzu na Nathan Sinkala
walijeruhiwa na kusababisha mgogoro kati ya shirikisho la soka la Zambia
na serikali ya Zambia.
Baada ya wachezaji hao kufanyiwa
ukaguzi mjini Lusaka, shirikisho la soka la Zambia likasisitiza kuwa
bado wanaweza kusafiri kwenda China kwa mchezo huo, lakini klabu ya
Mazembe ambako wachezaji hao hucheza soka ya kulipwa ikawataka kurejea.
Hatua hiyo ilisababisha serikali ya Zambia
kuingilia kati kwa kuwapokonya wachezaji hao pasi zao za usafiri ili
kuwazuia kwenda kuchezea klabu yao mjini Lubumbashi.
Hata hivyo, wachezaji walifanikiwa kuvuka mpaka na wanaaminika kuwa nchini DR Congo.
Shirikisho la soka la Zambia limeandikia barua
shirikisho la soka duniani Fifa, na kulalamika kuwa klabu ya Mazembe
haikuwaruhusu wachezaji hao kushirki majukumu yao ya kimataifa.
Zambia ilishindwa kwenye mechi hiyo ya kimataifa mjini Beijing
Zambia ambao ni mabingwa wa kombe la taifa
bingwa Afrika walikuwa wanashirki mechi yao ya kwanza wakiongozwa na
kocha wao mpya Patrice Beaumelle, ambaye alichukua usukani siku nane
zilizopita baada ya Herve Renard kucha kazi.
No comments:
Post a Comment