KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, October 7, 2013

VAN GAAL AMWITA KIUNGO WA NORWICH LEROY FER KUUNDA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA.

Kocha wa Uholanzi Lous Van Gaal amemuita kikosini kiungo aliye kwa mkopo katika klabu ya Norwich City Leroy Fer kwa ajili ya michezo miwli ya kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya Hungary baada ya Stijn Schaars Jonathan de Guzman kuondolewa kikosini kutokana na majeraha.

Jonathan de Guzman anasumbuliwa na msuli huku Stijn Schaars wa PSV akisumbuliwa na mguu.

Van Gaal amemuita Fer, ambaye ana michezo miwili tu ya kimataifa akicheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Ukraine mwaka 2010.

Bosi huyo wa Uholanzi pia aliwaita kwa mara ngingine tena Wesley Sneijder, Nigel de Jong Gregory van der Wiel wakati akitangaza kikosi kwa mara ya kwanza Septemba 25.

Uholanzi maarufu kama 'Orange' itakabiliana na Hungary kabla ya kucheza na Uturuki kwa ajili ya michezo ya kufuzu kombe la dunia huku tayari Uholanzi wakiwa na wamesha kata tiketi ya kucheza kombe la dunia nchini Brazil.

No comments:

Post a Comment