Rais wa chama cha soka nchini Liberia LFA Musa Bility amesema si kwamba ameaachana na ukosoaji wake wa sheria ya shirikisho la soka barani Afrika CAF
Bility nasema hayo wakati huu ambapo ndio kwanza anamaliza adhabu yake ya miezi sita ya kusimama katika shughuli za mpiwa miguu nchini kwake.
Mliberia huyo alihoji kifungu cha kuruhusu Rais wa CAF Issa Hayatou kuchaguliwa tena bila ya kupingwa mapema mwezi Machi.
Alifungiwa na Caf kama adhabu kutokana na kile kilicho elezwa kuwa alitumia nyaraka za siri .
Bility mara mbili alijaribu kukata rufaa katika mahakama ya kimataifa ya michezo CAS bula mafanikio.
No comments:
Post a Comment