KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, November 18, 2013

Kesho ni vita nchini Algeria na Misri. Nani wa kuungana na Nigeria, Cameroon na Ivory Coast. Mazingira yako hivi............soma taarifa hii.

Vita ya kuwania tiketi ya kufuzu kucheza kombe la dunia kwa mataifa kutoka barani Afrika imesalia baina ya Algeria dhidi ya  Bukina Fasoo na Misri dhidi ya Ghana michezo ambayo iyachezwa kesho Novemba 19.

Algeria watakuwa nyumbani wakiwakaribisha Burkina Fasoo walio mbele kwa magoli 3-2 na Algeria wakiwa wanaelekea katika mchezo huyo utakaochezwa uwanja wa Mustapha Tchaker mjini Blida huku nyuma wakisindikizwa na rekodi ya kufuzu fainali hizo mfululizo tangu mwaka 2002.

Pande hizo mbili zilikutana katika mchezo wa kirafiki ndani ya uwanja huo mwezi Juni ambapo Algeria walishinda 2-0 lakini hapo kesho mambo yanaonekana kuwa magumu kwa wenyeji hao ambao watalazimika kubadili matokeo ya 3-2 ya mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa mwezi uliopita mjini Ouagadougou.

Pamoja na mazingira ya kimatokeo kwasasa yakiwa hivyo bado Algeria wanapewa nafasi kubwa ya kukata tiketi licha ya mchezaji wa zamani wa Algeria Anthar Yahia kuvieleza vyombio vya habari kuwa mambo yote yatategemea kile kitakachokuwa kinatokea uwanjani.

The Stallions wa Burkina Faso waliwasili jana mji mkuu wa Algeria Algiers kabla ya kuelekea kwenye uwanja utakao tumika kwa pambano hilo huko Blida.

Kocha wa Algerian, Vahid Halihodzic amenukuliwa katika mkutano wake na waandishi wa habari akisema kuwa anajiamni kuwa atashinda na anafurahishwa na kiwango cha mchezo wa mkondo wa kwanza ambapo amesema kikosi chake maarufu kama Desert Foxes hawakuwa na bahati kwa kupoteza mchezo huo wa ugenini.

Kocha wa Burkinabe  Paul Put atakuwa na kiungo wake Alain Traore, kiungo mchezeshaji ambaye alikuwa na kipindi kizuri wakati wa fainali za mataifa ya Afrika katika mchezo wa kwanza kabla ya kukumbwa na majeraha na kumuweka nje katika michezo iliyosalia ya michuano hiyo.

Ushirikiano wa Traore na  Jonathan Pitroipa unawapa 'The Stallions' kujiamini zaidi na kocha Paul Put anaamini atafanya miujiza mjini Blida hiyo kesho.

Kwingineko

Misri itakuwa ikiingia uwanja w Air Defence kwa lengo la kubadili matokeo ya mchezo wa mkondo wa kwanza ambao walipigwa jumla ya mabao 6-1 dhidi ya Ghana mchezo uliochezwa mjini Kumasi.

Mchezo huo huko Cairo umekuwa ukizungumziwa kuwa pengine utakumbwa na ghasia huku hali ya wasiwasi juu ya usalama ikiwa mashani.

Ghana maarufu kama 'Blacks Stars' wamewasili Cairo saa mbili asubuhi ya leo na mchana wa leo kulitarajiwa kufanyika mkutano na waandishi wa habari katika uwanja ambao unatarajiwa mchezo huo kufanyika wakati ambapo kocha wa kikosi hicho Kwesi Appiah na nahodha Asamoah Gyan walitarajiwa kuongea na wanahabari.

Kocha wa Misri Bob Bradley, amejinadi kikosi chake kupigana kwa uwezo wake wote pamoja na kwamba kazi ya kubadili matokeo inaonekana kuwa ngumu.

 Amenukuliwa Bradley kupitia mtandao wa habari nchini Misri wa Al Ahram Sport akisema

"timu yetu imefanya kazi ngumu sana ya kukamilisha ndoto zetu na ni ndoto muhimu wa wamisri wote, nasikitika tumejiweka wenyewe katika ndoto ngumu itakuwa ngumu lakini bado tuna dakika 90 zaidi" 

Misri iliwashinda Zambia 2-0 katika mchezo wa kujiweka vizuri wiki iliyopita na kocha wa MaPharaohs Bob Bradley ameahidi kubadili matokeo ya Kumasi.

Michezo miwili ya kesho usiku itakuwa inakamilisha kuwapata wawakilishi watano (5) wa Afrika katika kucheza fainali za kombe la dunia nchini Brazil ambapo tayari Nigeria, Ivory Coast na Cameroon wamekwisha kukata tiketi zao mwishoni mwa wiki.

Ingawaje imekuwa ni kauli mbiu kwa Wamisri kuelekea katika mchezo wa kesho wakisema “Mission Impossible” bado kuna matumaini kwa MaPharaohs kwani watakuwa katika ardhi ya nyumbani.

No comments:

Post a Comment