KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, November 18, 2013

HARUNA NIYONZIMA ALIVURUGA KIUNGO CHA UGANDA CRANES, OWI ASHINDWA KUNG'ARA UWANJA WA NAMBOLE.

Kiungo wa timu ya taifa ya Rwanda maarufu kama 'Amavubi' akikoromeana na kiungo wa Uganda 'The Crane' Joseph Mpande huku mwamuzi kutoka Tanzania Israel Mujuni Nkongo aliyechezesha pambano hilo akitafuta suluhu baina yao.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes' Emmanuel Okwi (kushoto) akipambana na mchezaji wa Rwanda katika mchezo uliopigwa Jumamosi katika uwanja wa Namboole na kumalizika kwa sare 0-0.
Mchezaji wa Uganda Cranes Joseph Mpande akikabiliwa na mchezaji wa timu ya taifa ya Rwanda 'AMAVUBI' Emery Bayisenge (kulia) wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki ulipigwa katika uwanja wa Namboole Jumamosi na kumalizika kwa suluhu 0-0 katika mchezo huo wageni Rwanda walipata nafasi nyingi za wazi lakini walishindwa kumalizia vizuri.

Endapo kocha mkuu wa kikosi cha timu ya taifa ya Uganda Milutin ‘Micho’ Sredojevic atataka kuhakikisha kuwa kikosi chake kinatetea vema taji la michuano ya Chalenji ambayo itafanyika nchini Kenya, basi atalazimika kufanya kazi ya ziada kufanyamarekebisho ya haraka katika sehemu ya kiungo ya kikosi hicho.
Katika mchezo uliopita uliofanyika Jumamosi dhidi ya Rwanda Amavubi na kumalizika kwa suluhu ya 0-0 kiuongo wa timu ya Amavubi ambaye pia anachezea klabu ya Yanga ya Tanzania alionekana kutawala sana sehemu hiyo na kuwapa shida viungo wa Uganda akina Oscar Agaba, Joseph Mpande na Ayub Kisalita.
Wadadisi na wachambuzi wa mambo ya kisoka kutoka nchini humo pamoja na mashuhuda wa mchezo huo wamemtaka Micho Sredojevic kuongeza ufundi wake katika kiungo cha timu.
Pamoja na kuwaingiza uwanjani Tom Masiko, Muwadda Mawejje na Frank Kalanda katika sehemu hiyo katika kipindi cha pili bado kiungo chake kilionekana kupwaya na kukatika hovyo huku Niyonzima akiendelea kupasua sehemu hiyo ya kati atakavyo.
Maswali mengi ni juu ya mtazamo wa Micho wa kutaka kuwatumia wachezaji wanaocheza soka nchini Uganda katika michuano ya Chalenji( yaani local-based players) michuano ambayo inatarajiwa kuanza wiki mbili zijazo jijini Nairobi, ikiwa ni kuwajenga kwa ajili ya michuano ya CHAN nchini Afrika kusini mwezi Januari.
Katika mchezo hou mshambuliaji wa zamani wa Simba Emmanuel Okwi alipata nafasi mbili nzuri lakini alishindwa kukwamisha mpira wavuni.
Hata hivyo mshambuliaji huyo alikuwa akilazimika kutafuta mipira kuwanzia nyuma kutokana na kukosa sapoti kutoka sehemu ya kiungo kilichokufa.

No comments:

Post a Comment