KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, November 18, 2013

James Nandwa apewa mkataba wa miaka miwili kuiongoza AFC Leopards.

Siku moja baada ya kuiongoza vema AFC Leopards maarufu kama 'Ingwe' na kufanikiwa kutwaa taji la GoTV Shield Cup, kocha James Nandwa amepewa mkataba wa kudumu wa kuifundisha klabu hiyo kwa miaka miwili.
Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars ambaye alikuwa katika benchi la ufundi katika michuano ya mwaka jana ya Cecafa Challenge Cup mjini Kampala alichukuliwa kuiongoza Leopards mwezi Agosti kama kocha wa muda akichukua nafasi ya mtangulizi wake aliyetupiwa virago Mbeljiam Lucy Eymael na tangu wakati huo amekuwa akikiongoza vema kikosi hicho mpaka kushinda GoTV Cup lakini pia akikiwezesha pia kikosi hicho kushika nafasi ya pili nyuma ya waliokuwa mabingwa wa taji la ligi ya kenya Gor Mahia FC.
Mwenyekiti wa AFC Leopards Allan Kasavuli amesema wamemuongezea mkataba Nandwa wa kusali klabuni hapo.
"Tumefurahi kumaliza msimu na kikombe, lengo letu lilikuwa ni mafanikio ambayo tunayo kwa kumaliza katika nafsi ya pili katika 'Kenyan Premier League'.

“Nandwa has been instrumental in helping us do this and we want to work with him next year again to do even bigger things.”

Anatarajia kuiongoza Ingwe kuelekea katika mafanikio zaidi mwakani na kurejea katika soka la barani Afrika linalo ongozwa na Caf  na tukishiriki michuano ya Confederations Cup kwa mara ya kwanza kwa miaka mitatu.

No comments:

Post a Comment