KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, November 18, 2013

AFC LEOPARDS YATWAA TAJI LA Go TV Sheald

Bao pekee la Peter ‘Pinches’ Opiyo lilitosha kwa AFC Leopards kuwachapa wapinzani wao wakubwa kisoka nchini Kenya Gor Mahia FC katika mchezo wa fainali ya michuano ya Go TV Shield Cup mchezo uliopigwa uwanja wa Nyao jana Jumapili.
mshambuliaji huyo wa zamani wa Thika United ambaye yumo ndani ya orodha fupi ya wachezaji wanao wania tuzo ya kiungo bora wa ligi kuu ya Kenya KPL.
Alifunga goli hilo kunako dakika ya 53 kufuatia krosi nzuri ya Noah Wafula.
Pande zote mbili zilitengeneza nafasi mbalimbali za kufunga ambapo katika moja ya tukio kubwa la ushambuliaji ambapo mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Daniel ‘Mzee’ Sserunkuma alikataliwa kufunga goli huku shukrani za pekee zikielekzwa kwa mlinda mlango Martin Musalia.

Mlinda mlango wa Gor Mahia Jerim Onyango ameipongeza AFC Leopards lakini akilalamikia juu ya kupoteza nafasi nyingi kwa upande wao.

No comments:

Post a Comment