Klabu ya Tottenham imeelezwa kutojali afya kwa
kumruhusu mlinda mlango wake Hugo Lloris kucheza mechi dhidi ya Everton
baada ya kupoteza fahamu.
Lloris alipata jeraha kuchwani baada ya kuumizwa
Romelu Lukaku wa Everton aliyemjeruhi na mguu wake katika mechi ya
siku ya jumapili ambapo mpambano huo ulimalizika kwa kutoka suluhu ya
kutokufungana.
Kocha wa Spurs Andre Villas- Boas ametetea uamuzi wa kumuacha Lloris kuendelea na mchezo.
Nafasi ya mlinda mlango huyo awali ilitazamaiwa
kuchukuliwa na Brad Friedel.huku Lloris akitolewa nje ya uwanja lakini
alionekana yu tayari kuendelea na mchezo hatua iliyomfanya Villas-Boas
kutofanya mabadiliko yeyote.
Msemaji wa Taasisi ya afya ya Headway, Luke
Griggs amesema mchezaji anapopata jeraha kichwani ni wazi anaweza
kupoteza fahamu na ni muhimu wakapatiwa uangalizi wa karibu wa kitabibu.
Taasisi hiyo imesema kuwa mchezaji huyo
kuendelea na mchezo kunaweza kusababisha madhara zaidi kwa mchezaji,
hivyo alipaswa kuondolewa uwanjani mara tu baada ya kuumia na kupelekwa
hospitali kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.
No comments:
Post a Comment