Jopo
la wataalamu 20 walioteuliwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi linakutana kupanga mkakati wa kuonesha
jinsi Tanzania inavyoweza kushiriki Fainali za Afrika (AFCON)
zitakazofanyika mwaka 2015 nchini Morocco.
Kikao hicho maalumu (retreat) kitafanyika mjini Zanzibar kuanzia Desemba 6-8
mwaka huu. Jopo hilo litaongozwa na Mwenyekiti wa zamani wa Baraza la
Michezo la Taifa (BMT), Kanali mstaafu Idd Omari Kipingu.
Wengine
wanaounda jopo hilo linalohusisha pia makocha ni Dk. Mshindo Msolla,
Peter Mhina, Ayoub Nyenzi, Abdallah Kibaden, Pelegrinius Rutahyuga,
Kidao Wilfred, Salum Madadi, Juma Mwambusi, Ken Mwaisabula, Boniface
Mkwasa, Fred Minziro, Meja Abdul Mingange, Ally Mayay, Boniface Mkwasa
na Dan Korosso.
Wajumbe wengine wa jopo hilo wanatoka Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA).
No comments:
Post a Comment