![]() |
Newcastle inawaambia Arsenal kuwa Yohan Cabaye anauzwa kwa milioni £22. |
Newcastle imeitaka Arsenal kutenga paundi milioni £22 ili kuweza kumnyakuwa kiungo Yohan Cabaye katika kipindi cha dirisha dogo la usajili wa mwezi Januari.
Arsene
Wenger amekuwa katika harakati za kusaka kiungo mwenye kipaji katika sehemu ya kati ya kikosi chake na Cabaye anaweza kuihama klabu yake yenye maskani yake London ya kaskazini kama Arsenal itafikia kiwango hicho cha thamani ya mchezaji huyo.
Hizi zinaweza kuwa ni mbio za kumshindania kiungo huyo.
Cabaye amekuwa katika kiwango cha kuvutia hivi sasa ambapo alifunga bao lake la nne la msimu huu wakati kikosi cha meneja Alan Pardew kilipoishinda Crystal Place bao 3-0 Jumamosi iliyopita.
Arsenal ilianza kumfukuzia Cabaye tangu mwanzo wa msimu na hakuwepo katika mchezo wa ufunguzi wa msimu dhidi ya Manchester City.
Pardew
anadai kuwa kichwa chake kimekuwa kikiumizwa na nia ya Wenger juu ya Cbaye licha ya Newcastle
kukataa kumuuza kiungo huyo na walikataa ofa ya pauni milipni £10 huko nyuma.
Alifunga goli dhidi ya Manchester United wakati Newcastle iliposhinda Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1972.
Kwasasa Newcastle wako katika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi ya England alama sita nyuma ya vinara wa ligi hiyo Liverpool na Arsenal wenye alama 36 kila moja.
Vinara Arsenal hawajakata tamaa juu ya kipaji hiki ndani ya Premier League ambaye anahitaji kufanyiwa marekebisho kidogo na wanamtaka kwa ajili ya kujiimarisha zaidi katika duru la pili la msimu.
Newcastle bado wanasita kumuuza mchezaji huyu lakini wanawaambia Arsenal kuwa itawagharimu pauni milioni £22 kumsajili. Kwa bei hiyo itakuwa ngumu kukataa kwa mchezaji ambaye walimsajli kwa gharama ya pauni milioni £4 akitokea Lille ua Ufaransa mwaka 2011.
Je wanataka kariba ya wachezaji viungo kama hawa chini?
Jack Wilshere (22 appearance - 4 goals)
Aaron Ramsey (26 appearances - 13 goals)
Mikel Arteta (18 appearances - 1 goal)
Mathieu Flamini (16 appearances - 1 goal)
Mesut Ozil (21 appearances, 5 goals)
Santi Cazorla (19 appearances - 1 goal)
Tomas Rosicky (17 appearances - 0 goals)
Aaron Ramsey (26 appearances - 13 goals)
Mikel Arteta (18 appearances - 1 goal)
Mathieu Flamini (16 appearances - 1 goal)
Mesut Ozil (21 appearances, 5 goals)
Santi Cazorla (19 appearances - 1 goal)
Tomas Rosicky (17 appearances - 0 goals)
No comments:
Post a Comment