Mshambuliaji wa Tottenham, Emmanuel Adebayor, amesema kuwa wasimamizi wa klabu hiyo hawamuheshimu.
Adebayor, alifunga magoli mawili katika mechi
yake ya kwanza msimu huu pale Tottenham, ilipoilaza Southampton kwa
magoli matatu kwa mawili siku ya jumapili.
Lakini
mchezaji huyo mwenye umri wa miaka ishirini na tisa, hakujumuishwa
kwenye picha rasmi ya klabu hiyo na alikuwa akifanya mazoezi pekee waki
Andre Villas-Boas alipokuwa kocha.
''Ilikuwa ngumu sana, wakati nikija kufanya
mazoezi na kuona picha ya klabu yangu ambayo sijajumuishwa, hiyo
inamaanisha kuwa wao hawaniheshimu'' Alisema Adebayor.
Adebayor, aliichezea Tottenham kwa mkopo kutoka
klabu ya Manchester City mwaka wa 2011-12 na alifunga magoli kumi na
saba baada ya kuichezea mechi thelathini na tatu, kabla ya kujiunga na
Spurs kwa mkataba wa kudumu agosti mwaka wa 2012 kwa kitita cha pauni
milioni tano.
Lakini katika msimu wa mwaka wa 2012-13,
Adebayor alifunga magoli matano baada ya kucheza mechi thelathini na
sita na msimu huu alicheza dakika arubaini na tano pekee wakati wa
Villas-Boas alikuwa kocha.
Septemba mwaka huu, ilitangazwa kuwa Adebayor huenda akakihama klabu hiyo Januari mwaka ujao.
Lakini licha ya vilabu vingi kuonyesha nia ya kutaka kumsajili, mchezaji huyo hajaonesha dalili ya kutaka kuondoka.
Baada ya Villas-Boas, kufutwa kazi wiki
iliyopita na Tim Sherwood kuchukua mahala pake, kocha huyo mpya
alimjumuisha Adebayor katika kikosi cha wachezaji wake kumi na mmoja wa
kwanza.
Katika mechi yao dhidi ya West Ham siku ya
Jumatano Adebayor alifunga goli moja na mawili wakati wa mechi yao dhidi
ya Southampton siku ya Jumapili.
No comments:
Post a Comment