Jackson Martinez
Porto imepiga hatua moja mbele muhimu yenye lengo la kumbakisha mshambuliaji wa Kireno kutoka katika klabu ya Arsenal kwa kumpa ofa kubwa ya kusajili kwa minajili ya mpango wa kudumu.
Jackson
Martinez yuko katika rada ya mzee Arsene Wenger wakati wa usajili wa dirisha dogo la mwezi januari baada ya kuwa kufanya mambo makubwa tangu ajiunge na Porto ambapo amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 33 katika jumla ya michezo 37 aliyoichezea klabu hiyo tangu kuanza kwa msimu uliopita.
Aina yake ya umaliziaji imeonekana kuivutia Arsenal kiasi kuweka utashi wake huku Chelsea wakimuangalia kama ndio jibu sahihi la mbadala kufuatia kumkosa Wayne Rooney wakati wa kiangazi lakini puia inaarifiwa Liverpool nao kuhusishwa.
Hata hivyo Porto imejibu kwa kukaza uzi kwa hofu ya kumpoteza na kuelekea katika Barclays Premier
League ambapo sasa wameanza mazungumzo ya mpango mpya wa kudumu.
Mshambuliaji huyo mzaliwa wa Colombia mwenye umri wa miaka 27 atakuwa nje ya mkataba ifikapo 2016 na huenda akapewa ofa nono ya karibu asilimia 100 tofauti na ilivyo sasa ambapo inaarifiwa huenda akapewa malipo ya pauni £45,000 kwa wiki endapo Porto mabingwa wa Ureno watafanikiwa kumbakisha mpaka 2018.
Kipenzi cha mashabiki wa Porto Martinez amejijengea sifa ndani ya Ureno na Ulaya kwa ujumla.
Olivier Giroud
Martinez pengine angesajiliwa na Rafa Benitez kuelekea Napoli, lakini timu hiyo ya Serie A iliachana na mpango wa kusajili.
Akisajiliwa kutoka katika klabu ya Chiapas ya nchini Mexico, Martinez aliongoza kwa kufunga msimu uliopita akifunga magoli 26 magoli sita mbele ya anayemfuatia Lima wa Benfica na katika msumu huu akiwa ameshapachika wavuni magoli saba.
Arsenal
nao wanaamini juu ya umuhimu wake kwani uwepo wake katika safu ya ushambuliaji ambayo inamtegemea zaidi Olivier Giroud huenda ikaongeza chachu ya safu hiyo.
Hata hivyo wakala wake Luis Manso kwasasa yuko katika mazungumzo na viongozi wa Porto
na matumaini yao ni katika uhamisho wa mapema mwakani.
No comments:
Post a Comment