KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, December 5, 2013

Rais wa klabu ya Sevilla Jose Maria del Nido jela miaka saba.

 Rais wa klabu ya Sevilla Jose Maria del Nido amehukumiwa kwenda jela miaka saba kwa makosa ya ubadhirifu na upoteshaji wa haki.

Hukumu hiyo imemuhusu wakati huo akiwa ni wakili wa Rojiblancos supremo kati ya mwaka 1999 na 2003 akiwa wakili wa manispaa ya Marbella.

 Sambamba na meya wa zamani wa Julian Munoz, Del Nido alituhumiwa kwa kupanga mpango wa kujikusanyia fedha kutoka kwenye akaunti za umma.

Mnamo mwaka 2011,
Del Nido mwenye umri wa miaka 56 alishitakiwa kwa makosa hayo na kuhukumiwa kwenda jela kwa miaka saba na nusu na mahakama ya Malaga baada ya kukutwa na makosa ya ubadhirifu na upoteshaji wa haki.

Hata hivyo kupitia rufaa, mahakama kuu ilimuondolea kosa na kuondoa miezi sita ya hukumu yake.

Del Nido sasa analazimika kuachia ngazi kama Rais wa Sevilla baada ya miaka 11 ya utumishi wake huko Ramon Sanchez Pizjuan, ambapo katika kipindi cha uongozi wake klabu hiyo ilishinda mataji ya Uefa Cup, Europa League na Uefa Super Cup.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania ni kwamba Pepe Castro huenda akaziba pengo lake.

No comments:

Post a Comment