KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, December 5, 2013

CECAFA CHALLENGE CUP: Kilimanjaro Stars vs Uganda Cranes Jumamosi.

Khalid Aucho ameifungia goli lake la kwanza la mashindano timu yake ya taifa ya Uganda Cranes katika mchezo dhidi ya Sudan 1-0 uliopigwa uwanja wa Nyayo na kumaliza wakiwa vinara wa kundi C.

The Cranes wameongoza kundi baada ya kukusanaya alama tisa baada ya kushuka dimbani kwa michezo mitatu na magoli matano ya kufunga na kutokuruhusu nyavu zao kufungwa huku Sudan wakimaliza katika nafasi ya pili wakiwa na alama sita.
Uganda watakutana dhidi ya Kilimanjaro Stars katika mchezo wa robo fainali, ambao wamemaliza katika nafasi ya pili katika kundi B, mchezo ambao utapigwa Jumamosi ilhali Sudan wakijipanga kukutana dhidi ya Ethiopia.

Mchana wa leo Ethiopia ilimaliza katika nafasi ya pili katika kundi A baada ya kupoteza mchezo dhidi ya wenyeji Kenya. 
Timu hizo mbili zimemaliza hatua ya makundi kwa kuwa na alama sawa saba kila moja. 


Kuhusu mchezo baina ya Uganda na Sudan hakukuwa na kashikashi nyingi katika kipindi cha kwanza ambapo washambuliaji wa Uganda Daniel Sserunkuma, Emmanuel Okwi na Vincent Kayizzi hawakuweza kuona nyavu za wapinzani wao.


Lakini kocha Micho Sredojevic, aliwaingiza Brian Majwega kuchukua nafasi ya Sserunkuma wakati wa mapumziko ambaye alikwenda kuimarisha nguvu.

Goli la Uganda liliwekwa wavuni na kiungo wa Tusker FC ya Kenya Khalid Aucho kunako dakika ya 47 .

Baadaye mvua kubwa ikanyesha na kupelekea wachezaji kuanza kucheza mipira mirefu

No comments:

Post a Comment