Juhudi binafsi za mshambuliaji Michel Ndahinduka kunako za dakika ya 15 kabla ya mchezo kumalizika zimeiwezesha Amavubi Stars kukata kiu ya ushindi katika michuano ya chalenji ya cecafa msimu wa 2013 kutoka kundi C katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Jomo Kenyatta mjini Machakos.
Katika mchezo huo kocha Eric Nshamiyimana alimuanzisha benchi kiungo skipper Harunah Niyonzima lakini baada ya kuingia ndani ya dakika 30 alibadilisha hali ya mchezo.
Rwanda na Eritrea zote zilipoteza michezo yao ya kwanza ya hatua ya makundi kufuatia vichapo kutoka kwa Sudan and Uganda, ambao wanasonga mbele kwa hatua ya robo fainali.
No comments:
Post a Comment