Shangwe na hoi hoi za mashabiki wa mchezo wa American
football katika mji wa Seattle nchini Marekani zilisababisha kishindo
kikubwa cha makelele kusababisha tetemeko dogo la ardhi,kwa mujibu wa
wanasayansi.
Mashabiki waliokuwa na furaha waliruka
huku na huko lilipofungwa bao la mapema katika mchezo kati ya Seattle
Seahawks na New Orleans Saints.
Kituo kinachochunguza na kupima
mitetemeko ya ardhi The Pacific Northwest Seismic Network kilibaini
mtikisiko wa vipimo baina ya 1 na 2 ya nguvu za tetemeko la ardhi.
Seahawks walishinda mchezo huo katika uwanja wa CenturyLink Field kwa pointi 34-7.
Mkurugenzi wa kituo cha Pacific Northwest
Seismic Network John Vidale aliiambia CNN kwamba wanasayansi wake
walirikodi mitikisiko 5 tofauti ya ardhi wakati wa mchezo huo.
Hii si mara ya kwanza; kwani mwaka 2011
mashabiki wanaoshangilia walisababisha ardhi ya Seattle kutikisika
katika mchezo mwingine wa American Football.
Uwanja wa CenturyLink Field, ambao ni wazi pia uliweka rekodi ya dunia ya takwimu za Guinness World Record
No comments:
Post a Comment