Bayern Munich imeanza duru ya pili ya Bundesliga kwa ushindi wa mabao
2-0 dhidi ya Borussia Moenchengladbach jana Ijumaa baada ya mapumziko ya
wiki tano ya majira ya baridi.
Mario Goetze alifunga bao la kuongoza katika dakika ya saba ya mchezo,
wakati walinzi wa Moenchengladbach walipomuacha bila ulinzi na
kuupachika mpira wavuni , kabla ya Thomas Mueller kukamilisha ushindi wa
bayern kutokana na mkwaju wa penalti katika dakika ya 54.
Granit Xhaka wa moenchengladbach alitumia mkono kuusimamisha mpira katika mtafaruku golini na ndipo refa akaamua mkwaju wa penalti kwa Bayern.
Moenchengladbach ambayo ilikuwa haijafungwa nyumbani msimu huu, ilifanikiwa mara mbili kugonga mwamba wa goli la Bayern , wakati Max Kruse na patrick Herrmann waliopojaribu bahati yao dhidi ya kipa wa Bayern Manuel Neuer.
Matokeo hayo yameifanya Bayern kuendeleza ubabe wa kutofungwa katika Bundesliga kwa michezo 42 na sasa imepanua mwanya wa uongozi hadi point 10 ikifuatiwa na Bayer Leverkusen ambayo inacheza leo jioni dhidi ya Freiburg.
Mabingwa hao hata hivyo wana mchezo mmoja zaidi ambapo watacheza dhidi ya Stuttgart siku ya Jumatano ili kutimiza michezo 18 ya ligi ya Ujerumani Bundesliga hadi sasa.
"Iwapo tutacheza kama tulivyocheza leo tutakuwa mabingwa wa Ujerumani", amesema rais wa Bayern Uli Hoeness.
Mshambuliaji mashuhuri wa Bayern Mario Mandzukic hakuwamo katika kikosi hicho jana. Mkurugenzi wa sporti wa Bayern Munich Matthias Sammer amesema kabla ya mchezo huo kuwa mshambuliaji huyo kutoka Croatia hajafanya mazowezi vya kutosha.
Hakutaka kusema hata hivyo iwapo usajili wa Robert Lewandowski kutoka Borussia Dortmund kwa ajili ya msimu ujao una athari yoyote katika hilo.
Matokeo ya michezo ya leo

Finished
|
Freiburg
| - |
Bayer Leverkusen
| (1-2) | ||||||
Finished
|
Wolfsburg
| - |
Hannover 96
| (1-1) | ||||||
Finished
|
Nurnberg
| - |
Hoffenheim
| (2-0) | ||||||
Finished
|
Borussia Dortmund
| - |
Augsburg
| (1-0) | ||||||
Finished
|
VfB Stuttgart
| - |
Mainz 05
| (1-1) | ||||||
25/01 20:30
|
Eintracht Frankfurt
| - |
Hertha Berlin
|
Wakati huo huo Lukas Podolski aliweka mpira wavuni katika kipindi cha kwanza jana na kuisaidia Arsenal kuirarua Coventry ya daraja la tatu kwa mabao 4-0 katika mchezo wa duru ya nne ya kombe la FA.
Katika mchezo ambao Arsenal iliutawala toka mwanzo hadi mwisho, Podolski aliwainua mashabiki wa Arsenal katika dakika ya 15 kwa kufunga bao safi baada ya kumegewa pasi safi na Mesut Ozil. Aliongeza bao la pili kwa kichwa kunako dakika ya 27 ya mchezo.
Katika mchezo mwingine wa kombe la FA jana Ijumaa , Nottingham Forest ilitoka sare ya bila kufungana na Preston.
No comments:
Post a Comment