KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, January 16, 2014

Manchester United: Anderson Luís de Abreu Oliveira atimkia Fiorentina kwa mkopo.Anasema Fellaini kamchongea

Anderson akijiandaa kupanda mwewe kuelekea Italia kumalizana na Fiorentina
Kiungo aliyekuwa hana nafasi na aliyekuwa hatakiwi kuendelea kuwepo Manchester United Anderson Luís de Abreu Oliveira ameelekea nchini Italia kujiunga na Fiorentina akitangulia kufanyiwa vipimo vya afya yake ikiwa ni mpango wa uhamisho wake wa mkopo wa kujiunga na kikosi hicho kinacho shiriki ligi kuu ya nchini Serie A. 

Kiungo huyo raia wa Brazil amewaeleza marafiki zake kuwa alikuwa akisaka uhamisho wa kudumu kujihakikishia muda zaidi wa kucheza soka lakini United ndio waliomkwamisha kwa kumuondoa klabu hapo kwa mkopo.

Anderson alionekana Frankfurt mapema asubuhi ya leo akiwa akiwa katika zoezi la kuunganisha ndege akitokea Manchester mpango wake wa uhamisho ukitarajiwa kukamilishwa hapo kesho Ijumaa.
With the arrival of Marouane Fellaini, Anderson has found opportunities hard to come by this term
Tangu kuwasili kwa Marouane Fellaini, Anderson alijua wazi kuwa nafasi yake ya kucheza itakuwa ngumu katika kipindi hiki.

  Kuanguka kiwango kwa Anderson na winga Luis Nani kunawafanya wachezaji hao kuondolewa kwa mkopo Old Trafford. Anderson ameichezea United michezo minne tu msimu huu.

Alijiunga na United mwaka 2007 akitokea Porto kwa pauni milioni £20 na kufanya michezo 179 akifunga magoli tisa.

Kwa upande wao Fiorentina wana majeruhi ya akina Giuseppe Rossi na Mario Gomez hivyo wamekuwa wakiwasiliana na vilabu vya Premier League kusaka washambuliaji huku kutoka AS Roma wakimkodolea macho Marco Borriello na kutoka Juventus wachezaji wawili Mirko Vucinic Fabio Quagliarella.
Out: David Moyes has decided that Anderson is the first that needs to be cleared out from United's midfield
TOKA: David Moyes aliamua tangu mapema kuwa Anderson ndiye mchezaji wa kwanza kufagiwa kutoka sehemu ya kiungo


Kuondoka kwa Anderson kutapelekea United kusonga mbele zaidi katika harakati za kumnasa Paul Pogba kurejea kundini Old Trafford.
Mfaransa huyo aliyeihama Manchester na kujiunga na Juventus mwaka 2012, atawagharibu kiasi cha pauni milioni £40 na tayari amesha angaziwa hivi karibuni na David Moyes.

Mchezaji mwingine ambaye yuko mguu ndani mguu nje ni mlinzi wa pembeni Fabio.

Cardiff City inamnyemelea mlinzi huyo licha ya madai ya wakala wake kuwa atasalia United mpaka kiangazi.

No comments:

Post a Comment