KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, January 18, 2014

Seeb Club 0-0 Coastal Union uwanja wa Seeb Club.

Coastal Union ya Tanga ‘Wagosi wa Kaya’ leo wametoka suluhu ya bila mabao dhidi ya Seeb SC inayoshiriki ligi kuu ya Oman.
 
Mchezo wa leo unakuwa ni mchezo wao wa nne tangu kuwasili nchini Oman Januari 9, kwa ziara ya wiki mbili kujiandaa na ligi mzunguko wa pili Tanzania Bara.
 
Coastal Union, imeonyesha uhai katika kipindi cha pili ambapo kipindi cha kwanza walishindwa kuonyesha makeke yao huku wachezaji wa Seeb wakitumia zaidi sehemu ya kiungo, na kuwapa wakati mgumu Wagosi kushindwa kumiliki mpira.

Kipindi cha pili Seeb Club, walifanya mabadiliko kwa kutoa wachezaji wawili wa ndani na mlinda mlango. Coastal Union waliendelea kucheza bila kufanya mabadiliko.
 
Katika dakika za awali kipindi cha pili Seeb walionyesha uhai na kulisumbua sana lango la Wagosi, lakini kufuli za Juma Nyoso na Othman Tamim ziliendelea kuwa imara kuulinda mlango wa Shaaban Kado.
 
Aidha ilipofika dakika ya 76, kocha Yusuf Chipo alifanya mabadiliko ya haraka haraka kwa kutoa wachezaji wanne na kuingiza wanne wengine zikiwa zimesalia dakika 15 mchezo kumalizika.
 
Alianza kutoka Othman Tamim akaingia Abdi Banda, baadae akatoka Danny Lyanga akaingia Mohammed Miraji. Halafu zikiwa zimesalia dakika chache mchezo kuisha alitoka Atupele Green akaingia Suleiman Kassim Selembe, na kufanya mabadiliko ya mwisho kwa kumuingiza Abdullah Othman ‘Ustadh’ akatoka Yayo Kato.
 
Listi ya leo ilikuwa: Shaaban Kado, Hamadi Juma, Othman Tamim, Juma Said ‘Nyoso’, Mbwana Kibacha, Jerry Santo, Ally Nassor ‘Ufudu’, Danny Lyanga, Atupele Green, Haruna Moshi ‘Boban’, na Yayo Kato.
 
Coastal Union tangu iwasili Oman imeshacheza mechi nne, imeshinda mechi mbili kati ya Oman Club na Al Mussannah kwa mabao 2-0 kila mechi. Halafu ikafungwa bao 1-0 na Fanja Club, leo imetoka suluhu ya bila kufungana na Seeb Club.
COASTAL UNION
18 JANUARI, 2014
MUSCAT, OMAN

No comments:

Post a Comment