Sehemu ya kuingilia ndani ya uwanja kumbukumbu ya Sokoine |
![]() |
Sehemu ya kuchezea ya uwanja wa Ally Hassani Mwinyi mkoani Tabora |
Hii ndio sehemu ya kuingilia uwanjani sehemu ya VIP ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine ulioko mkoani Mbeya |
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeteua maofisa wanaoanza leo
(Januari 14 mwaka huu) kukagua viwanja 19 vitakavyotumika kwa mechi za
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Ukaguzi
huo pia unahusisha viwanja ambavyo Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
ilizuia mechi za VPL na FDL kuchezwa mpaka hapo vitakapokuwa vimefanyiwa
marekebisho ili kukidhi sifa za kutumiwa kwa mechi hizo.
Viwanja
vinavyokaguliwa ni Ali Hassan Mwinyi (Tabora), CCM Kirumba (Mwanza),
Jamhuri (Dodoma), Jamhuri (Morogoro), Kaitaba (Bukoba), Kambarage
(Shinyanga), Kumbukumbu ya Karume (Musoma) na Kumbukumbu ya Samora
(Iringa).
Kumbukumbu
ya Sokoine (Mbeya), Lake Tanganyika (Kigoma), Mabatini (Pwani),
Majimaji (Songea), Mbinga (Mbinga), Mkwakwani (Tanga), Mwadui
(Shinyanga), Wambi (Mufindi, Iringa), Sheikh Kaluta Amri Abeid (Arusha),
Umoja (Mtwara) na Vwawa (Mbozi).
Vyama vya mpira wa miguu vya mikoa husika na mameneja wa viwanja husika wanatakiwa kuwapa ushirikiano wakaguzi hao kutoka TFF.
No comments:
Post a Comment