Swansea City imemfuta kazi kocha wake Michael Laudrup
na kumpa nahodha wa timu hiyo Garry Monk kuiongoza katika mechi ya ligi
dhidi ya wapinzani wake Cardiff City Jumamosi ijayo.
Taarifa hizo zinajiri siku moja tu baada ya
mwenyekiti wa kilabu hiyo Huw Jenkins kupuuzilia mbali tetesi kuwa
walikuwa wamezungumzia mustakabali wa Laudrup.
Uvumi ulikuwa umesambaa kuhusu hatma ya Laudrup baada ya Swansea kushindwa kwa mabao 2-0 dhidi ya West Ham Jumamosi iliyopita.
Hiyo ilikuwa mara ya sita timu hiyo kupoteza
katika mechi nane za Ligii kuu ya Uingereza na kuiacha na alama mbili tu
juu ya timu ambazo zitateremshwa katika ligii hiyo.
Monk alikuwa amepigiwa debe kuchukua nafasi hiyo ikiwa mojawapo ya njia za kuboresha kikosi hicho.
No comments:
Post a Comment