MTIBWA SUGAR,
SIMBA KUUMANA MOROGORO
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya 16
kesho (Februari 5 mwaka huu) kwa mechi tano huku Mtibwa Sugar ikiikaribisha
Simba kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kiingilio
katika mechi hiyo ambayo itakuwa ya kwanza kuchezwa kwenye uwanja huo wenye
uwezo wa kuchukua watazamaji 10,000 tangu uanze mzunguko wa pili wa VPL kitakuwa
sh. 5,000. Jonisia Rukyaa kutoka Bukoba ndiye atakayechezesha mechi hiyo.
Mechi
nyingine za ligi hiyo ni Tanzania Prisons vs Coastal Union (Sokoine, Mbeya),
Mgambo Shooting vs Ruvu Shooting (Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers vs Oljoro
JKT (Ali Hassan Mwinyi, Tabora) na JKT Ruvu vs Ashanti United (Chamazi, Dar es
Salaam).
TFF YASITISHA MATUMIZI
YA TIKETI ZA ELEKTRONIKI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesitisha matumizi ya tiketi za elektroniki kwenye
viwanja vyote vyenye huduma hiyo ili kutoa fursa ya kufanyika tathmini ya kina
kabla ya kuendelea tena.
Uamuzi
huo umefikiwa kwa kuzingatia sababu mbalimbali baada ya kikao kati ya
Sekretarieti ya TFF na maofisa wa benki ya CRDB kilichofanyika jana (Februari 3
mwaka huu) katika ofisi za Shirikisho.
Tathmini
hiyo inafanyika ili kubaini changamoto zilizojitokeza na kuzitafutia ufumbuzi
kabla ya kuendelea tena na matumizi hayo, kubwa ikiwa ni hadhari iliyotolewa na
vyombo vya Usalama juu ya misongamano inayotokea uwanjani kutokana na
kutokuwepo mtiririko mzuri wa uingiaji.
Tayari
zipo changamoto za wazi ikiwemo uelewa wa washabiki wa jinsi ya kununua na
kutumia tiketi hizo, milango michache ya kuingilia uwanjani na washabiki wengi
kununua tiketi dakika za mwisho hivyo kuchangia misongamano.
40 KUNG’AMUA
VIPAJI UBORESHAJI TAIFA STARS
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeteua kikosi cha makocha 40 kutoka sehemu
mbalimbali, Tanzania Bara na Zanzibar ili kung’amua vipaji katika mpango wa
kuboresha timu ya Taifa (Taifa Stars).
Makocha
hao ambao watafanya kazi hiyo katika michuano maalumu ya mikoa wanatakiwa kuripoti
katika ofisi za TFF siku ya Jumamosi (Februari 8 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwa
ajili ya kupewa maelekezo zaidi.
Walioteuliwa
ni Abdallah Hussein (Kilimanjaro), Abdul Mingange (Dar es Salaam), Ali Bushiri
(Zanzibar), Ali Mayay (Dar es Salaam), Ally Mtumwa (Arusha), Ayoub Selemani
(Zanzibar), Boniface Pawasa (Dar es Salaam), Dan Korosso (Mbeya), Dk. Mshindo
Msolla (Dar es Salaam) na Edward Hiza (Morogoro).
Elly
Mzozo (Dar es Salaam), Fred Minziro (Dar es Salaam), George Komba (Dodoma), Hafidh
Badru (Zanzibar), Hamimu Mawazo (Mtwara), Idd Simba (Mwanza), Jabir Seleman (Zanzibar),
John Tegete (Mwanza), Juma Mgunda (Tanga) na Kanali mstaafu Idd Kipingu (Dar es
Salaam).
Kenny
Mwaisabula (Dar es Salaam), Khalid Abeid (Dar es Salaam), Madaraka Bendera
(Arusha), Madaraka Selemani (Dar es Salaam), Mbarouk Nyenga (Pwani), Mohamed
Mwameja (Dar es Salaam), Musa Kissoki (Dar es Salaam), Nicholas Mihayo (Dar es
Salaam), Patrick Rweyemamu (Dar es Salaam) na Peter Magomba (Singida).
Peter
Mhina (Songea), Salvatory Edward (Dar es Salaam), Salum Mayanga (Morogoro), Sebastian
Nkoma (Dar es Salaam), Sekilojo Chambua (Dar es Salaam), Shaban Ramadhan
(Zanzibar), Steven Nemes (Dar es Salaam), Sunday Manara (Dar es Salaam), Tiborowa
Jonas (Dar es Salaam), Yusuf Macho (Dar es Salaam), Zamoyoni Mogela (Dar es
Salaam),
QUALITY GROUP
YAIPIGA JEKI TFF
Kampuni
ya Quality Group Limited imetoa sh. milioni 10 kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kwa ajili ya kuunga mkono mikakati ya shirikisho la katika kuendeleza
mpira wa miguu nchini.
Mchango
huo wa Quality Group utatumika katika programu mbalimbali za kuendeleza mpira
wa miguu nchini ambapo tunaishukuru kampuni hiyo kwa kuunga mkono mikakati
yetu.
No comments:
Post a Comment