Mshabiki
mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi akidaiwa kukutwa na tiketi bandia kwenye
mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Mbeya City iliyochezwa jana
(Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Matei
Cosmas (28) ambaye ni mkazi wa Buza Njiapanda Kitunda, Dar es Salaam
amefunguliwa jalada namba CHA/IR/900/2014 kwenye Kituo cha Polisi Chang’ombe
akidaiwa kupatikana na tiketi bandia.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo asubuhi (Februari 3 mwaka huu) limeamkia
Kituo cha Polisi Chang’ombe kusaini hati ya maelezo dhidi ya mtuhumiwa.
Ni
imani ya Shirikisho kuwa mtuhumiwa atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za
nchini.
Tunatoa
mwito kwa washabiki wa mpira wa miguu kuepuka kununua tiketi kutoka mikononi
mwa watu, kwani kufanya hivyo ni kosa. Tiketi zinauzwa kwenye sehemu maalumu
zenye chapa ya TFF.
No comments:
Post a Comment