KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, February 3, 2014

Mrehemu Omari Changa azikwa jijini Dar es Salaam, TFF yatoa salamu za rambirambi

Mwili wa marehemu Omari Changa, mshambuliaji wa zamani wa vilabu za Yanga, Afrikan Lyon, Moro United , JKT Ruvu na vilabu vingine  ukisitiriwa makaburini jioni ya leo. Marehemu alikutwa amefariki dunia alfajiri ya jana katika eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam huku chanzo cha kifo chake kikishindikana kujulikana. Mungu ailaze roho ya Omari Changa mahali pema peponi Amina. Picha kwa hisani ya salehejembe.com.
Marehemu Omari Changa (watatu kutoka kushoto waliosimama) enzi za uhai wake akiwa na kikosi cha Ruvu Shooting.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa mchezaji wa Vijana, Moro United na Yanga, Omari Changa kilichotokea juzi (Februari 1 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

Msiba huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu kwani Changa wakati wake uwanjani akichezea timu mbalimbali alitoa mchango mkubwa ambao tutaukumbuka daima.

TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Changa, klabu ya Moro United na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Katika maziko TFF itawakilishwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Kidao Wilfred, na imetoa rambirambi ya sh. 200,000.

No comments:

Post a Comment