KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, March 22, 2014

AIBU DARAJANI: Mourinho aongeza jeuri mbele ya Arsene Wenger kwa kumtwisha zigo la mabao Darajani

Penati ilitolewa baada ya Alex Oxlade-Chamberlain kuzuia mpira kwa mkono uliopigwa na Eden Hazard kuelekea katika mwamba wa pembeni wa lango lakini kadi nyekundu ikatolewa kwa Gibbs
Mchezo wa 1000 kwa meneja wa Arsenal, Arsene Wenger akiwa ni katika benchi la ufundi la klabu hiyo umekuwa shubiri kwa mzee huyo mfaransa wakati vijana wake waliokuwa 10 uwanjani walipo pokea kichapo cha mabao 6-0 kutoka kwa Chelsea katika mchezo wa ligi kuu ya England.

Arsenal walikuwa nyuma kwa mabao mawili hadi kufikiwa dakika ya saba ya mchezo kufuatia mabao ya mapema ya Samuel Eto'o na Andre Schurrle ambao walifunga mabao hayo kwa mipira ya kukimbiza yaani 'counter-attacking'.

Bao la tatu lilikuwa ni mkwaju wa penati uliotokana na mpira wa kushika wa Alex Oxlade-Chamberlain akiwa ndani ya eneo la hatari penati ambayo iliwekwa kwenye kamba na Eden Hazard huku mabao mshambuliaji Oscar akifunga mabao mawili kabla ya Mohamed Salah kuongezea machungu kwa washika mitutu wa jiji la London.

Shambulizi la mshambuliaji aliyetokea benchi Mohamed Salah lilikamilisha misumari katika jeneza la Arsenal hii ambao walikuwa ughaibuni darajani.

Hata hivyo jambo lisilo la kawaida ni pale kadi nyekundu ya moja kwa moja ilipotolewa kwa Kieran Gibbs kufuatia mpira wa mkono uliohcezwa na Oxlade-Chamberlain kipindi cha kwanza cha mchezo. 

Huu ni ushindi mkubwa kwa meneja wa Chlesea Jose Mourinho ndani ya Premier League akiwa meneja wa Chelsea na pia ni mara ya kwanza kwa Chelsea katika historia ya Chelsea kupata ushindi mkubwa dhidi ya wapinzani wa jiji la London.

Licha ya Oxlade-Chamberlain kumwambia mwamuzi wa mchezo Marriner kuwa yeye ndiye aliyefanya kosa hilo lakini bado kadi hiyo ikaelekezwa kwa Gibbs.

No comments:

Post a Comment