KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, March 29, 2014

Ligi ya England: Mashabiki wa United wamepinga watumia ndege kufikisha ujumbe wa kumkataa Moyes

Wayne Rooney amefunga magoli mawili katika mchezo ambao Manchester United ilipigana ikitokea nyuma kimatokeo dhidi ya Aston Villa licha ya matakwa ya mashabiki wa klabu hiyo kupinga kuendelea kuwepo katika nafasi ya umeneja kwa David Moyes huku wakitaka afukuzwe kazi.
Ndege iliyokuwa na bango la kitambaa lilikuwa na ujumbe la kumpinga Moyes ambalo lilizomewa na baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo wakati likipita juu ya uwanja wa Old Trafford dakika ya pili ya mchezo.

Ashley Westwood alipiga Free-kick ambayo iliwaweka mbele Villa lakini Rooney akapiga piga bao la kuswazisha kwa United halafu akaandika bao la pili kwa njia ya mkwaju w penati kufuatia Leandro Bacuna kumfanyia madhabi Juan Mata.

Mata aliandika bao la tatu murua kabla ya Javier Hernandez kukamilisha kwa bao la nne katika dakika za majeruhi.

Mshambuliaji wa Villa Christian Benteke alikosa nafasi mbili nzuri katika kipindi cha pili.

Ujumbe wa ndege uliunganishwa na mashabiki ambao ulisomeka 
"Wrong One - Moyes Out"
Lakini hata hivyo haukupokewa vizuri na mashabiki ndani ya kiwanja ilipotokea ngege hiyo.
The fly-by protest calling for Manchester United manager David Moyes to be sacked

No comments:

Post a Comment