KLABU ya Barcelona
imethibitisha kumsajili mchezaji nyota chipukizi Alen Halilovic kutoka
klabu ya Dinamo Zagreb. Nyota huyo anayecheza nafasi ya kiungo
mshambuliaji amekuwa akiwindwa na vilabu mbalimbali barani Ulaya ikiwemo
Manchester City, lakini ni Barcelona waliofanikiwa baada ya kutuma
ujumbe wao nchini Croatia kumaliza dili hilo.
Kinda huyo mwenye umri wa
miaka 17 ambaye anatokana na matunda ya shule ya vipaji ya Dinamo
amesaini mkataba wa miaka mitano kwa ada ya euro milioni 2.2.
Akihojiwa
Halilovic ambaye anafananishwa na Messi mdogo amesema ni ngumu kupata
maneno ya kuzungumza jinsi anavyojisikia lakini anaishukuru sana Dinamo
ambao atawapenda siku zote kwa kumfikisha hapo alipo sasa.
Pia kinda
huyo aliwashukuru makocha katika shule ya Dinamo waliomfundisha mpaka
kufikia sambamba na mashabiki ambao mara zote wamekuwa nyuma yake.
No comments:
Post a Comment