KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, April 5, 2014

YANGA SASA WATUMIA KANUNI YA 9 KIPENGELE CHA 21 KUDAI ALAMA TATU ZA MEZANI ZA MGAMBO SHOOTING

Klabu ya Yanga imewasilisha malalamiko Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwa mshambuliaji wa Mgambo Shooting Stars ambaye alicheza dhidi yao katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Mohamed Neto si raia wa Tanzania na hana Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).

Ingawa malalamiko hayo yamewasilishwa nje ya muda (time barred), TFF imeyapokea na itayawasilisha kwenye Kamati husika kwa ajili ya kupitiwa na baadaye kutolewa uamuzi.

Kwa mujibu wa kanuni, malalamiko yote kuhusu mchezo yanatakiwa kuwasilishwa ndani ya saa 24 baada ya mchezo kumalizika.

Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom 2013/2014

Kanuni ya 9,
Kipengele cha 21:
Iwapo Itadhibitika bila kujali kukatwa au kutokatwa Rufaa, kupitia taarifa za Kamisaa ama kwa njia yoyote kuwa timu imechezesha mchezaji/wachezaji ambao si halali au ni batili kiusajili (non qualified) timu hiyo itapoteza mchezo na ushindi kupewa timu pinzani.

No comments:

Post a Comment