KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, April 14, 2014

Ibrahima Traore nyota wa kimataifa wa Guinea aelekea Monchengladbach ya Ujerumani

Borussia Monchengladbach imemsajili nyota wa kimataifa wa Guinea rahima Traore akitokea katika klabu ya VfB Stuttgart kwa ajili ya msimu ujao wa ligi. 

Winga huyo mwenye umri wa miaka 25 anajiunga akiwa mchezaji huru na ameingia mkataba wa miaka minne na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya nchini Ujerumani Bundesliga.

"Ibrahima Traore ni winga mwenye kasi ambaye ataongeza nguvu katika ushambuliaji na kuifanya kuwa na wepesi na utulivu" mkurugenzi wa michezo wa Monchengladbach Max Eberl amesema.
"Anakuja kama mchezaji huru na tunafuraha ameamua kujiunga nasi"
Traore ni mmoja wa wachezaji ambeya amepeleka mabadiliko katika kikosi cha Stuttgart msimu huu ambapo mabingwa hao wa zamani wa Bundesliga wamepigana kuepuka kushuka daraja ikiwa bado wana michezo minne iliyosalia.
Kabla ya kujiunga na Stuttgart, mzaliwa huyo wa Ufaransa aliwahi kuichezea Augsburg pia alipata wakati akaichezea Hertha Berlin.
Amecheza jumla ya michezo 71 Bundesliga na kufunga magoli sita.
Monchengladbach wako katika nafasi ya sita huku wakikodolea macho nafasi ya ushiriki wa michuano ya Europa League.

No comments:

Post a Comment