KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, April 14, 2014

Licha ya kuipelekea Arsenal kwenye fainali ya FA Cup, hasira za mashabiki kwa Wenger zaongezeka

Uungwaji mkono kwa meneja Arsenal kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo kunaarifiwa kuwa kumezidi kupunguz kwa takribani asilimia 30 kuanzia Jumamosi licha ya klabu hiyo kuifunga  Wigan kwa mikwaju ya penati na kutinga fainali ya FA Cup.

Licha ya kuwapa Gunners nafasi nzuri zaidi ya kushinda taji la kwanza katika kipindi cha miaka 9,lakini namna ya walivyopata ushindi dhidi ya waliokuwa mabingwa watetezi wa taji hilo la FA kumeshusha wasiwasi miongoni kwa mashabiki wa klabu hiyo na hizi zikiwa ni data zilizo andaliwa na Pitch Social Insight.

Uchambuzi huo kupitia chombo hicho cha uchambuzi wa kimtandao umegundua kuwa kuwa Wenger aliingia katika mchezo huo akiwa na asilimia 60 za uhakika wa mahaba ya mashabiki walioonekana kupitia mtandao wa Twitter, lakini mazungumzo yaliyomuhusu mfaransa huyo kuanzia saa 12 jioni ya mchezo yalifikia asilimia 23.4 na inaonekana kuzidi kupungua kufuatia ushindi wa mchezo wa nusu fainali hiyo uliamuliwa kwa njia ya mikwaju ya penati.

Kiwango cha hasira kuelekea kwa Wenger kilipanda mpaka kufikia asilimia 61.3 wakati wa mchezo.

No comments:

Post a Comment