KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, May 3, 2014

Maecedes wanataka kufanya kweli katika msimu huu wa mashindano

Mercedes wanasema wanataraji kuongeza ufanisi na ubora wao katika mashindano yajao licha ya kutawala mbio za magari tangu kuanza kwa msimu.

Lewis Hamilton na Nico Rosberg walishinda mbio nne za mwanzo wa msimu, huku magari yao yakidhihirisha ubora katika kona ya pili ukilinganisha na magari ya wapinzani wao.

Bosi wa michezo wa Mercedes Toto Wolff amenukuliwa akisema
"Dhamira yetu ni kuongeza faida tuliyo anza nayo, tulifurahia katika mbio za mwishoni.
Lewis Hamilton cruises to win in China
Hamilton akivumisha gari huko China kabla ya kushinda.

"Wapinzani wetu si haba hawakuwa mbali kupunguza mwanya wa umbali" 

Dereva wa Ferrari Fernando Alonso ndiye aliyekuwa karibu na madereva wa Mercedes katika kupigania ushindi. 

Mhispania huyo alikuwa nyuma kwa alama 38 dhidi ya Rosberg, ambaye aliongoza mbio baada ya ushindi na alishika nambari tatu akishika namba mbili nyuma ya Hamilton katika mbio nne zilizoshindaniwa.

No comments:

Post a Comment