KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, May 3, 2014

Valdado ataka Casillas kumalizia michezo ya ligi kusaka ubora dhidi ya Atletico

Kocha wa zamani wa Real Madrid Jorge Valdano amesema Iker Casillas anapaswa kuchukua nafasi ya Diego Lopez katika michezo ya ligi kuu ya soka nchini Hispania 'La Liga' ili ajiweke safi kabla ya fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya ndugu zao Atletico Madrid.

Bosi wa Madrid Carlo Ancelotti amekuwa akizungusha zamu za walinda mlango wake msimu mzima huku Lopez akianza katika michezo ya ligi 'Primera Division' na Casillas akicheza michezo ya Copa del Rey na ligi ya mabingwa.

Kwa muendelezo huo wa sera yake hiyo ni wazi kuwa Casillas atadaka katika fainali itakayopigwa jijini Lisbon Ureno ikiwa ni mechi yake ya 22 katika msimu huu.

Kumekuwepo na wito kutoka vyombo vya habari vya nchini HIspania ambavyo vimekuwa vikitaka mlinda mlango huyo kumalizia michezo minne ya ligi kujihakikishia ubora kabla ya fainali inayotarajiwa kupigwa May 24, fainali ambayo inafananishwa na 'derbi'.

Valdano, ambaye aliwahi kufanya kazi kwa karibu na Casillas wakati huo akiwa mkurugenzi wa michezo ndani ya Estadio Santiago Bernabeu kuanzia 2009 mpaka 2011, amelieleza gazeti la El Larguero kwamba kwa mlinda mlango kuwa nje ya mchezo kwa mwezi mzima kabla ya mchezo mkubwa kama huo si wazo zuri.

No comments:

Post a Comment