Mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon Samuel Eto'o amwita Jose Mourinho' PUMBAVU' kufuatia bosi huyo wa Chelsea kuhoji uhalali wa umri wake mapema msimu huu.
Mourinho alihoji hilo mbele ya waandishi wa habari mwezi Februari mjini Switzerland akiamini kuwa Eto'o anaweza kuwa na umri mkubwa zaidi ya alio nao sasa.
Mourinho alihoji hilo mbele ya waandishi wa habari mwezi Februari mjini Switzerland akiamini kuwa Eto'o anaweza kuwa na umri mkubwa zaidi ya alio nao sasa.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33 alionekana kujibu hilo katika mchezo aliofunga goli uliofuata ambapo alishangilia goli lake kwa kushika mgongo kuashiria maumivu ya utu uzima.
Hata hivyo Eto'o ambaye kwasasa yuko nje ya mkataba na klabu hiyo yenye maskani yake Stamford Bridge ameng'aka juu ya kauli hiyo ya Mourinho na kusisitiza kuwa anaweza kucheza soka katika kiwango cha juu mpaka baadaye sana.

"Leo, nina umri wa miaka 33 amini hivyo na si kwasababu pumbavu kaniita mzee" Mshambuliaji huyo raia wa Cameroon amesema hayo alipokuwa akiongea na mtandao wa africanfootball.com.
"Unaweza kuona jinsi mzee alivyokuwa bora kwa vijana nyota. Baadhi waliaamini kuwa anaelekea kustaafu soka nchini Marekani au mashariki ya kati, lakini nilirejea katika ligi ya mabingwa Ulaya na ninaelekea kucheza ligi hiyo ya mabingwa.
"Wapi? sitakuambia."

Eto'o anaelekea kucheza fainali nyingine ya kombe la dunia akiwa na kikosi cha Cameroon mwezi ujao ambapo mchezaji huyo bora mara nne wa Afrika anadhani anaweza kuendelea na kuvunja rekodi za akina Lothar Matthaus na Antonio Carbajal za kucheza fainali tano za kombe la dunia.
"Naendelea kucheza kwasbabu niko fiti kimwili na kiakili najisikia safi"
"Naendelea kucheza kwasbabu niko fiti kimwili na kiakili najisikia safi"
"Hivyo nakwenda kombe hili la dunia na lijalo ambapo nitakuwa na umri wa miaka 37. Wengine walifanya hivyo wakiwa na umri wa miaka 42, hivyo naweza kucheza fainali nyingine mbili zijazo."
No comments:
Post a Comment