Wachumba wakiwa na furaha: Je unapata tabu kugundua wachumba hawa wanasapoti timu gani? |
Ni kama kubakia njia panda: Utafanya nini kama kuna mchezo mkubwa unachezwa lakini pia umealikwa katika harusi katika muda huo huo wa mchezo? Je utakwenda na redio kwa kusikilza matangazo ya mchezo huo ukiwa harusini? au utaendelea na matukio ya harusi kwasababu tu ya ukubwa wa siku hiyo kwa wawili hao?
Nchini Kenya wachumba waliamua kupamba tukio la harusi yao kwa kutumia nakshi za rangi nyekundu na nyeupe pamoja pia ikitumika jezi na bendera za klabu ya Manchester
United katika Keki na mavazi ya harusi ambapo tukio lilionekana kama linahusisha watu kutoka OLd Trafford kwa mashetani wekundu
Bibi harusi amevalia vazi la shela kama kawaida likipata nakshi ya kibanio cha rangi nyekundu lakini bwana harusi ameonyesha dhahiri mapenzi yake kwa United kwa kuvalia jezi yenye ujumbe wa kuelezea kuwa hilo lilikuwa ni tukio la Harusi
Keki imepambwa kwa Ice nyekundu ikiwa na nembo ya Chevrolet ambayo ni logo ya vifaa vya United msimu wa 2013-14.
Gari la maharusi aina ya Mercedes limeonekana likiwa na rangi za United licha ya rangi ya silver.
Hili ndilo gari la maharusi
Jionene mwenyewe bendera ya Manchester United
No comments:
Post a Comment