KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, September 7, 2014

Mchezo wa Yanga na Big Bullets ya Malawi washindwa kufanyika uwanja wa Taifa hii leo

Mchezo wa Yanga dhidi ya Big Bullets ya Malawi uliokuwa ufanyike jioni ya leo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam haufanyika tena kutoka na kile kilichoelezwa kuwa wageni wamekwawa maeneo ya Mzuzu nchini Malawi.

Akiongea na Rockersports katibu wa chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam Msanifu Kondo ambaye chama chake ndicho kilichokuwa kimeratibu mchezo huo amesema Big Bullets ambao zamani walikuwa wakitambuliaka kama 'Butter Bullets' kabla ya kuitwa tena 'Bakili Bullets' wamekwama nchini Malawi eneo la Mzuzu wakiwa njiani kuelekea jijini Dar es Salaam kwa mchezo huo.

Kondo amewataka radhi wapenzi wa soka nchini waliokuwa tayari wamejipanga kuelekea uwanja wa Taifa kushuhudia mchezo huo na kwamba bado juhudi zinaendelea za kuhakikisha Yanga inapata mchezo mwingine ama na timu hiyo au timu nyingine ya nje ya nchi kabla ya mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Azam fc septemba 14.  

Huu ungekuwa ni mchezo wa pili wa kimataifa kwa Yanga baada ya Jumatano kuitandika Thika United ya Kenya kwa bao 1-0 liliofungwa na mshambuliaji Mbrazil Gelson Jaja tangu kurejea kutoka visiwani Zanzibar ilikokuwa imeweka kambi yake ambako ilicheza michezo mitatu na kushinda yote.
Gilson Jaja akipongezwa ba wachezaji wenzake Oska Joshua, Haruna Niyonzima baada ya kufunga bao pekee la Yanga dhidi ya Thika United ya Kenya Jumatano

No comments:

Post a Comment