Mwanaridha Rita Jeptoo wa Kenya amepatikana kuwa alitumia dawa za kusisimua misuli zilizopigwa marufuku.
|
Mwanariadha wa mbio za marathon
kutoka Kenya Rita Jeptoo amepatikana kuwa alitumia dawa za kusisimua
misuli zilizopigwa marufuku.
Jetoo alifanyiwa uchunguzi nchini
Kenya mnamo mwezi Septemba wiki mbili kabla ya kushinda mbio za Chicago
marathon kwa mwaka wa pili mfululizo.
Chama cha riadha nchi Kenya AK kimelezea kughadhabishwa na matokeo hayo.
Jeptoo
aliye na umri wa miaka 33 alitarajiwa kukabidhiwa kitita cha dola nusu
milioni mjini New York siku ya Jumapili kutokana na ushindi huo lakini
sasa sherehe hizo zimahairishwa. |
No comments:
Post a Comment