Maafisa wa polisi nchini Afrika kusini wakipiga saluti jeneza la marehemu Senzo Meyiwa wakati umati wa wananchi wa Afrika kusini wakifuatilia.
Maafisa wa pilisi wakiwa wamebeba jeneza lililofunikwa kwa bendera ya taifa ya Afrika kusini katikati ya uwanja.
Pichani anaonekana mjane wa Meyiwa Mandisa Meyiwa (kulia), baba yake Sam (wapili kutoka kushoto) na mama yake Ntombifuthi (watatu kutoka kushoto)
Meyiwa, akiwa katika picha wakati akiitumikia timu ya taifa dhidi ya Congo Oktoba 15. Mlinda mlango huyo ameagwa na wachezaji wenzake na mshabiki
Picha iliyochukuliwa January 2013 ikionyesha Rais wa Afrika kusininPresident Jacob Zuma (kushoto) akipiga picha na Senzo Meyiwa wakati alipotembelea timu ya taifa mjini Soweto
Maelfu kwa maelfu walionekana hii leo wakibubujikwa na machozi huku macho yao yakiwa na rangi nyekundu wakiwa wamevalia jezi nyeusi na wengine nyekundu wakisema buriani Senzo Meyiwa katika mji wa Durban.
Huzuni ilitawala watu wakilia kwa uchungu wakimlilia mlinda mlango huyo aliye uwawa akiwa na umri wa miaka 27 ambapo jeneza lake lilizungushwa uwanjani huku watu wakipuliza vuvuzela na kuimba nyimbo za kisoka.
Mjane wa Meyiwa |
Wengi waliohudhuria mazishi hayo waliungana kwa pamoja ndani ya uwanja wa Moses Mabhida akiwemo mjane wa Meyiwa, wanasiasa,wachezaji wa mpira wa miguu, watu mashuhuri na maarufu na kutoa salamu zao za mwisho kwa mpendwa wao.
Meyiwa, alipigwa risasi Jumapili iliyopita, baada ya majambazi kuingia nyumbani
mwa mpenzi wake karibu na Johannesburg.
Mtuhumiwa wa mauaji ya Meyiwa
alifikishwa mahakamani Ijumaa na alishitakiwa kwa mauaji dhidi ya mlinda
mlango huyo maarufu nchini Afrika Kusini.
Kifo cha Meyiwa
kilisababisha mshituko mkubwa nchini Afrika Kusini na yameonyesha
kiwango cha juu cha uahlifu wa kutumia nguvu nchini humo.
Mazishi yanafanyika katika uwanja wa mpira wa miguu wa Moses Mabhida Stadium katika mji wa Durban nyumbani kwa Meyiwa.
Senzo Meyiwa alionekana kama kivutio katika mchezo wa mpira miongoni mwa wananchi wa Afrika Kusini.
Wengi wa waombolezaji wamevaa fulana zenye picha ya Meyiwa, mtu ambaye alikuwa kivutio kikubwa kimichezo.
Mazishi
ya mwanamichezo mwingine shujaa wa Afrika Kusini, bingwa wa zamani wa
dunia wa mbio za mita 800 Mbulaeni Mulaudzi, pia yatafanyika Jumamosi.
Mulaudzi aliuawa katika ajali ya gari kabla ya kifo cha Meyiwa.
Rais Zuma ameamuru bendera ya taifa ipepee nusu mlingoti siku ya Jumamosi ili kumuenzi mlinda mlango huyo wa timu ya taifa.
Mechi kati ya timu za Orlando Pirates na Kaiser Chiefs katika ligi ya Afrika Kusini imeahirishwa baada ya kifo cha Meyiwa.
Senzo Meyiwa alikuwa nahodha na mlinda mlango wa timu ya Afrika Kusini, Bafana Bafana.
Mamlaka
ya soka nchini humo wametangaza mchezo wa timu ya taifa ya Afrika
Kusini wa kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya Sudan
ifanyike Durban.
Polisi wamesema Ijumaa kuwa mtuhumiwa wa mauaji ya Meyiwa alitambuliwa katika gwaride la utambuzi.
Mtuhumiwa
huyo, Zanokuhle Mbatha, mwenye umri wa miaka 25, anakabiliwa na
mashitaka ya mauaji na ujambazi wa kutumia silaha na anatarajiwa
kufikishwa tena mbele ya mahakama Novemba 11.Polisi wametangaza zawadi
kwa mtu atakayewezesha kupatikana kwa taarifa zaidi kuhusu shambulio
hilo ili kuwanasa watuhumiwa wengine.
Meyiwa alipigwa risasi akiwa nyumbani kwa mchumba wake huko kusini mashariki ya jiji la Johannesburg Jumapili iliyopita |
Mwanamke akibubujikwa na machozi wakati wa sherehe ya kuuaga mwili wa mpendwa wao Meyiwa. |
No comments:
Post a Comment