KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, August 17, 2010

MILNER KUELEKEA MANCHESTER CITY KUBADILISHWA NA STEVEN IRELAND PAMOJA NA PESA JUUManchester City wakubali ada ya Milner
Manchester City wamekubali mpango wa kubadilishana mchezaji kwa kuunganisha na cash ama pesa mpango ambao una muhusu kiungo wa Aston Villa James Milner..
Milner mwenye umri wa miaka 24 mchana wa leo alitarajiwa kufanyiwa vipimo huko Eastlands na kaiungo wa City Stephen Ireland anatarajiwa kuondoka Eastland kuelekea upande wa pili huko Villa Park.
Meneja wa City Roberto Mancini anamatumaini kumalizia taratibu zote za uhamisho hapo kesho.
City wamekuwa wakimshawishi nyota huyo wa kimataifa wa uingereza tangu kuanza kwa majira ya kiangazi huku wakianza kifanya hivyo kabla ya kuanza kwa fainali za kombe la dunia. Ada ya uhamisho imeripotiwa kuwa ni pauni milioni £20.
Milner katika mchezo wake wa mwisho kuitumikia Villa ilikuwa ni mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya uingereza Premier League jumamosi ambapo villa waliibika na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya West Ham.
MHISPANIA KUWA KOCHA WA SIMBA WASIOSHINDIKA CAMEROON HUYU NI JAVIER CLEMENTE ANACHUKUA NAFASI YA PAUL LE GUEN Mamlaka nchini Cameroon zimethibitisha kocha mpya wa timu ya taifa ya Camerron ambaye ni Javier
Kocha mzaliwa wa Hispania ametangwa rasmi kuwa kocha mpya wa kikosi cha timu ya taifa ya Camerron Indomitable Lions
Baada ya siku kadhaa za kuwepo taarifa za kuthibitishwa kwa Javier Clemente kuwa kocha mpya wa Cameroon taarifa ambazo hapo kabla ziliarifiwa na vyombo vya habari vya Hispania na baadaye kupita ukimya toka kwa mafia wa shirikisho la kandanda la nchini Camerron FECAFOOT hatimaye meneja wa zamani wa klabu ya Athletico Madrid ametangazwa leo kuwa kocha mpya wa Cameroon kwa mujibu wa “Journal du Cameroun”.
Kocha huyo mwenye umri wa maika 60- atakuwa akisaidiana na makocha nyota wawili wa zamni wa simba hao wasioshindika hawa ni mshambuliaji wa zamani wa RC Lens François Omam-Biyik ambaye sasa anaumri wa miaka 44 ambaye atakuwa ni msaidizi wake wa moja kwa moja na mlinda mlango wa zamani wa FC Metz na Camerron Jacques Songo’o ambaye naye ana umri wa miaka 46 ambaye anakuwa kocha wa makipa.

Kwa mujibu wa taarifa zilizo patika kutoka ndani ya shirikisho la kandanda la Cameroon FECAFOOT zimesema kuwa kuchelewa kutangazwa kwa jina la kocha mpya kumetokana na kutokuwepo na maakubaliano ya kimsingo na kocha huyo mpya ikiwa ni pamoja na muda wa mkataba na makazi yake. FECAFOOT ilikuwa ikitaka wampe mkataba wa miaka minne na maskani yake yawe nchini Camerron lakini hata hivyo hilo limeshindikana na kwamba Clemente amefanikisha mpango wake wa kusaini mkataba wa miaka miwli na katika kipindi hicho maskani yake yawe nusu Camerron na nusu nyingine kwa Hispania .
Cameroon wanatarajia kuanza kampeni za kuwania kufuzu mataifa ya Afrika mwaka 2012 wiki chache zijazo wakiwa pamoja na mataifa ya DR Congo, Mauritius and Senegal katika kundi E.



NIKOLAS ANELKA NJE YA TIMU YA TIMU YA TAIFA YA UFARANSA MICHEZO 18 ILHALI NAHODHA PATRICE AKIFUNGIWA MICHEZO MITANONicolas Anelka kukiona cha moto asimamishwa jumla ya michezo 18 ya ufaransa
Nicolas Anelka amesimamishwa kutokucheza jumla ya michezo 18 ya timu ya taifa ya ufaransa adhabu ambayo imetolewa na shirikisho la kandanda nchini Ufaransa (FFF) hii ikiwa ni kutokana na matendo yake ya utovu wa nidhamu katika kambi ya Ufaransa katika fainali ya kombe la dunia zilizo malizika nchini Afrika kusini.
Anelka mashambulia mwenye umri wa miaka 31alirejeshwa nyumbani baada ya mzozo kuibuka kati yake na aliyekuwa kocha wa ufaransa katika fainali hizo Raymond Domenech jambo ambalo lilipelekea mgomo wa chini kwa chini wa mazoezi kwa timu nzima kupinga maamuzi ya kurejeshwa kwa Anelka.
Wakati FFF wakitoa adhabu hiyo kwa Anelka aliyekuwa nahodha Patrice Evra yeye amekumbana na adhabu ya kusimama kwa michezo mitano kama nahodha kushindwa kuweka hali sawa.
Franck Ribery amesimamishwa kwa michezo mitatu na Jeremy Toulalan mchezo mmoja.
Eric Abidal ni miongoni mwa wachezaji watano wa timu hiyo iliyokuwa Afrika kusini ambao walikutana na kamati ya nidhamu na kufanikiwa kuikwepa adhabu hiyo.





MESUT OZIL AJIUNGA NA REAL MADRID AKITOKEA WERDER BREMEN Real Madrid yathibitisha kunasa saini ya nyota wa ujerumani Mesut Ozil
Real Madrid imekamilisha kupata saini ya nyota wa kombe la dunia mjerumani Mesut Ozil ambaye anatokea from Werder Bremen.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 amekuwa katika hali nzuri kimchezo tangu ujerumani kutinga katika hatu ya nusu fainli ya kombe la dunia na kuanza kuwavutia makocha wa vilabu mbalimbali duniani hasa vya ulaya.
Vilabu viwili hivyo vimekubaliana kimsingi ada ya uhamisho ya EURO milioni 15 huku akiwa amesaliwa na mwaka mmoja wa mkataba wake.
Kesho Ozil atafanyiwa vipimo vya afya huko Madrid.
Nyota huyo anayetumia guu la kushoto anakuwa mchezaji mpya wa Real Madrid chini ya Jose Mourinho akiwa ni mchezaji wa sita kufuatia kusajliwa kwa Khedira, Ricardo Carvalho,Pedro Leon,Sergio Canales na Angel di Maria.




BELLAMY AREJEA NYUMBANI KATIKA KLABU YA CARDIF AKITOKEA MANCHESTER CITY Craig Bellamy akamilisha uhamisho kuelekea Cardiff City
Craig Bellamy hatimaye amekamilisha uhamisho wake wa kuelekea katika ligi ndogo ya nchini Uingereza maarufu kama Championship katika klabu ya Cardiff City kwa mkopo wa muda mrefu akitokea Manchester City.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 amekaririwa na mtandao wa klabu yake mpya akisema
"nimefurahishwa na kurejea nyumbani Cardiff.
"najisikia raha kuvalia t-shirt ya klabu hii na kuichezea klabu hii ambayo nilikuwa ninaisupoti tangu nikiwa mdogo."
Cardif maarufu kama “Bluebirds” wanatarajia kuutangazia uma kupitia mkutano na waandishi wa habari ambao utafanyika hivi punde jumamosi na jumamosi nahodha huyo wa Wales atakuwa katika kikosi cha Cardif kitakacho kabiliana dhidi ya Doncaster Rovers katika ligi ya nyumbani.
Akikaririwa Bellamy anasema
"natarajia kufanya kazi kwa nguvu zangu zote nikiwa na timu yangu mpya nikiwa na wenzangu ili kuiletea mafanikio na kuleta mafanikio katika ligi ya Championship hasa tukianza na mchezo wa jumamosi .

No comments:

Post a Comment