KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, August 22, 2010

MKENYA DAVID RUDISHA AVUNJA REKODI YA DUNIA HUKO UJERUMANI
Mkimbiza upepo toka nchini Kenya David Rudisha amefanikiwa kuvunja rekodi ya dunia ya mita 800 kwa wanaume kwa kutumia muda wa dakika moja sekunde 41.09 katika mbio za IAAF World Challenge zilizo fanyika jumapili hii huko Berlin nchini ujerumani.

Rekodi ya awali ilikuwa ni dakika moja na sekunde 41.11 ambayo ilikuwa inashikiliwa na mwanaridha mwenye asili ya mataifa mawili ya Denmark na Kenyan aliyezaliwa Kenya Wilson Kipketer aliyoiweka mwaka 1997 mjini Cologne.

Akikaririwa na BBC 5 live Rudisha amesema
"najisikia furaha na ni kama naota kuwa mtu wa kwanza kukimbia kwa muda huu wa dakika moja na sekunde 41".

"nilikua nakimbia haraka na nilikuwa najua kuwa nina rekodi ya dunia lakini sikuwahi kushinda katika mashindano makubwa bado.

"sasa ni wakati kuangalia hilo na kushinda medali katika michuano ya dunia mwaka ujao na ninataka kuwa mshindi katika mashindano ya Olympic . That is my focus from now on."

Rudisha alifanikiwa mara moja kufikia katika hatu ya nusu fainali mwaka jana katika shindano kama hilo katika uwanja huo huo wa mji mkuu wa ujerumani wa German capital's Olympic Stadium.

Katika hatua nyingine katika jiji la mji mkuu wa Belgian wa Heusden-Zolder mwezi July, mshindi huyo wa Afrika alifanikiwa kukimbia kwa kutumia muda wa dakika moja na sekunde 41.51

Wakenya wengine Boaz Kiplagat Lalang na Abraham Kiplagat walikuwa nyuma kwa zaidi ya sekunde tatu kila mmoja katika nafasi ya pili na ya tatu.

No comments:

Post a Comment