KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, August 16, 2010

RIO FERDINAND KUENDELEA KUTAMIGWA MWEZI MMOJA ZAIDI NA LIGAMNENT MTAZAME PICHANIMlinzi Rio Ferdinand wa mashetani wekundu ataendelea kusalia nje ya uwanja kufuatia kuendelea kukabiliwa na maumivu kwa mujibu wa kocha wake Sir Alex Ferguson.
Nahodha huyo wa uingereza alikuwa katika wakati mgumu miezi miwili iliyopita ambapo alikuwa katika kazi kubwa ya kuhakikisha analitibu jeraha lake ambalo lilimuweka nje ya mashindano ya kombe la dunia.
Ferguson aliwahi kunukuliwa july 25 kuwa mlinzi wake huyo mwenye umri wa miaka 31 angerejea dimbani baada ya wiki sita , na kumuweka nje katika michezo ya mwanzoni mwa msimu na vilevile akitarajiwa kukosekana katika mchezo wa awali wa kutafuta nafasi ya kuelekea kwenye fainali za Euro 2012 dhidi ya Bulgaria september 3 na baadaye dhidi ya Switzerland siku nne baadaye.
AKIKARIRIWA Furguson anasema
"Rio is nowhere near, no. anaonekana bado na nadhani anaweza kuwa nje ya uwanja kwa karibu mwezi mzima "


RYAN GIGGS ANAJIPANGA KUFUIFUNDISHA MAN UNITED AU TIMU YA WALES MANCHESTER UNITED NEWS
Giggs anajipanga kuwa meneja wa Manchester United
Ryan Giggs ameshajiweka katika mazingiya ya kuweza kuwa meneja wa Manchester United au Wales wakati ukifika way eye kustaafu kucheza soka.
Giggs ambaye kwa sasa ana miaka 36 akicheza katika nafasi ya winger amekuwa ni mwenye kupata heshima mbalimbali za klabu hiyo kwa miaka 20 aliyokuwepo klabu na kwasasa ameanza kuonekana kuanza kuzungumzia juu ya mpango wake wa kutaka kufuata nyayo za za wenzake waliowahi kupita Old Trafford akina Steve Bruce, Mark Hughes, Roy Keane na Bryan Robson ambao walianza kazi ya kufundisha muda mfupia baada ya kutundika daruga.
Akikaririwa mwenyewe anasema
"lengo langu ni kuwa meneja wa aidha Manchester United au Wales japo kuwa sijui kama nitafanana maeneo hayo ngoja kwanza nistaafu.
Anasema mpira wa miguu ni sehemu ya maisha yake na angependa kufuata nyayo za akina Roy Keane .

No comments:

Post a Comment