KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, August 19, 2010

VITALI KLITSCHKO KUTETEA TAJI LAKE LA WBC DHIDI YA SHANNON BRIGGS OCTOBAR HUKO UJERUMANI
KATIKA PICHA JUU VITALLI KUSHOTO NA BRIGGS KULIA WALIPOKUTANA HUKO CARDIF
Bingwa wa dunia wa taji la uzito wa juu linalotambuliwa na WBC king Vitali Klitschko amethibitisha kutetea mkanda wake dhidi ya mmarekani Shannon Briggs katika pambano ambalo litapiganwa kunako October 16 huko Hamburg nchini ujerumani.
Pambano hilo sasa linamaliza matumaini ya bondia kutoka nchini uingereza bingwa wa taji la ubingwa wa dunia unaotambuliwa na chama cha ngumi cha dunia WBA David Haye anmbaye alikuwa na haja ya kutaka kukutana na Klitschko raia wa Ukrain ndani ya mwaka huu.
Akikaririwa Klitschko anasema
"Briggs ana uzoefu mkubwa na amepigana vizuri mapambano yake tofauti na nilivyopigana mimi.
Klitschko ambaye kwasasa ana umri wa miaka 39 amecheza mapambano s 40 na kupoteza mawili ilhali Briggs mwenye umri wa miaka 38 amecheza mapambano 51 na kupoteza matano na kwenda sare pambano moja.
Kwa Klitschko hii itakuwa ni mara yake ya tano kutete mkanda wake tangu kumchapa Samuel Peter mwezi October mwaka 2008 na kutwaa taji la WBC licha ya wakati Fulani mwaka 2004 kustaafu kwa muda.
Kwa bingwa huyo wa dunia wa WBC mara ya mwisho kuzichapa ilikuwa nio dhidi ya mpoland Albert Sosnowski mwezi May 2010, wakati ambapo mmarekani toka jijini New York Briggs yeye mara ya mwisho alizichapa na kumshinda Rob Calloway mwezi May.
Kaka yake na Klitschko huyu ni Wladimir Klitschko yeye atatetea mikanda yake ya uzito wa juu ya IBF, WBO na IBO dhidi mnigeria Peter katika pambano litakalo pigwa huko Frankfurt September 11.

No comments:

Post a Comment