KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, October 18, 2010

FIFA YACHANGANYIKIWA NA WAJUMBE WALIOTAKA RUSHWA KABLA YA KUPIGA KURA YA NANI KUANDAA KOMBE LA DUNIA 2018/2022


AMOS ADAMU MJUMBE ANAYETAKA RUSHWA HUYU HAPA CHINA Shirikisho la kandanda duniani FIFA limesema litachunguza kama chembechembe za rushwa zilizo jitokeza katika harakati za kuomba kuandaa michuano ya kombe la dunia kufuatia taarifa kuzagaa katika vyombo vya habari nchini uingereza kuwa kuwa kuna wajumbe wawili wa kamati ya utendaji ya shirikisho hilo ambao wamepewa rushwa kuuza kura yao kwa moja ya taifa linalo taka kuandaa fainali hizo
Sunday Times limeonekana kuwa na picha ya mmoja wa wajumbe toka Nigeria Amos Adamu na Rais wa Oceania Football Confederation Reynald Temarii wa Tahiti wakiomba ngawira kufanikisha mpango huo.
Wanahabari wamekuwa wakijaribu kuomba jitihada za makusudi zifanyike kwa makampuni ya Marekani kuwezesha fainali za kombe la dunia zinarejea nchini Marekani na kwamba pesa isitumike kubadili hali ya hewa.

Akikaririwa mwenyekiti wa mpango wa marekani wa kamati ya kuandaa na kuomba maandalizi ya kombe la dunia ambaye pia ni Rais wa shirikisho la la kandanda nchini Marekani Sunil Gulati anasema

"Sunday Times katika taarifa yake hii leo imeweka wazi kashfa hiyo lakini pia inarejesha kuonyesha mkazo kwa Marekani kutaka kuandaa bila ya hata kuunganishwa na mpango wa rushwa ulioripotiwa hii leo jambo ambalo sasa tunawaachia FIFA na sisi hatuna na kuongeza."

Adamu na Temarii ambao wamehusishwa na kutaka rushwa hata hivyo hawakuweza kufikiwa kuombwa mawazo yao juu ya hilo ni miongoni mwa wajumbe 24 ambao wana kura katika kikao cha kuamua nani wa kuandaa fainali za kombe la dunia mwaka 2018 na 2022 katika kikao ambacho kitafanyika December 2 huko Zurich Uswiz yaliko makao makuu ya FIFA.

"FIFA na kamati ya nidhamu ya FIFA wamekuwa wakifuatilia juu ya mchakato wa mpango wa maandalizi ya kuandaa kombe la dunia kwa mwaka 2018 na 2022 na wanaendelea kufanya hivyo “
Imekaririwa taarifa ya FIFA
FIFA tayari imeomba taarifa na maelezo kamili yanayo husiana na tukio hilo na inasubiri taarifa kamili.
"In any case, FIFA watabaini ukweli juu ya hilo basi itaamua nini cha kufanya"
Mrekani imeomba kuandaa fainali za kombe la dunia kwa mwaka 2022 maombi ambayo yanazihusu pia Australia, Japan, South Korea na Qatar.
Lakini kuelekea katika fainali za 2018 Uingereza na Russia wamekuwa wakipigana vikumbo kuitaka nafasi hiyo sambamba na mataifa ya Belgium na olland wakitaka kuandaa kwa pamoja kama ilivyo kwa Hispania na Ureno
Adamu alipigwa picha akizungumza na wana habari huko London kuwa anataka dolari za kimarekani $800,000 ili akaweke artificial turf katika viwanja vya Nigeria.

Adamu amewaambia wana habari kuwa anataka pesa hizo kwanza yeye mwenyewe na kusema
"Certainly if you are to invest that, that means you also want the vote."
Wakati mambo hayo yakitokezea mwezi uliopita huko Cairo Mrekani ilikuwa ikiwania kuandaa fainali za kombe la dunia kwa miaka yote miwili yaani 2018 na 2022 lakini ijumaa iliyopita Mrekani umetangaza kujitoa katika mchakato wa kuandaa fainali za 2018.
Adamu ame-offer "guarantee" kuwa ataipigia kura marekani katika mpango wa 2018 lakini pia katika 2022.
Tukiachana na Adam gazeti hilo la Sunday Times limeweka mtandao ambao wewe msikilizizaji unaweza kupata sauti jamaa mwingine muamba rushwa Temarii ambaye aliomba dolari za kimarekani milioni 2.3 ambazo zitasaidia kujenga football academy huko Auckland.
Lakini pia kuna mataifa mengine mawili ambayo hayakuwekwa wazi yameahidi kumpa makamu wa Rais wa FIFA dolari za kimarekani milioni 10 mpaka 12 wa ajili ya shirikisho la kandanda la Oceania.

No comments:

Post a Comment