WAHANGA WA MACHIMBO YA CHILE WAKARIBISHWA SANTIAGO BERNABEU NA OLD TRAFFORD NA KATIKA MICHEZO YA NEW YORK MARATHON
Wachimbaji madini wa Chile walioishi chini ya ardhi kwa muda wa siku 69, wamekaribishwa uraiani kwa kwenda kushuhudia michezo ya soka huko ulaya na Latin American na hata kushiriki katika michezo ya New York City Marathon.
Rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez amewaalika wachimbaji hao 33 kutembelea Santiago Bernabeu ilhali klabu ya Manchester United ikifanya kufanya hivyo.
Wahanga hao wa machimbo ya madini huko Chile waliookolewa wameonekana kufurahishwa kufanya ziara hiyo ya kutembelea vilabu hivyo vikubwa pamoja na kutembelea katika NYC Marathon .
Wahanga hao waliokolewa jumatano kwa kukamilisha idadi ya mtu wa mwisho kuokolewa baada ya kuwa chini ya ardhi kwa siku takribani 69 baada ya kuwa chini ya ardhi kwenye urefu wa futi 2,000 baada ya machimbo hayo kubomoka Aug. 5.
Mwasisi wa Manchester United Bobby Charlton motto wa mwenye mgodi ameripotiwa akituma ujumbe uliorikodiwa akiwa aalika Old Trafford.
Mchawi wa chenga wa Argentina na kocha wa zamani wan chi hiyo Diego Maradona ametuma ujumbe akisema kuokolewa kwa wahanga hao ni miujiza ambayo ipo na tuko pamoja nao
Naye kocha wa Boca Juniors Claudio Borghi anasema tungependa kukaa nao meza moja na kunywa na chai.
Mmoja wao ambaye aliwahi kucheza soka la kulipwa ameeleza kuwa angependa kusheherekea kwa kuelezea uwezo wake wa kucheza soka huku mwingine Omar Reygadas akioonyesha kitambaa cha klabu ya Colo Colo
Perez ametuma t-shirts 33 zilizo sainiwa za Madrid kwa wahanga hao na ambazo zina nmaandishi yanayo someka "Have strength, miners."
Perez pia anasema pia ametuma kitabu chenye picha za wachezaji wa zilizo sainiwa na wachezaji hao na kusaini mwaliko wa kuelekea Bernabeu.
Baada ya wahanga hao kuokolewa mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania David Villa ambaye amezaliwa katika familia ya wachimbaji huko Hispania jimbo la Asturias ametuma t-shirts mbili za klabu zilizo sainiwa zikiwa na maandishi "Miners, keep your spirits up."
No comments:
Post a Comment