KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, October 18, 2010

Jose Manuel De La Torre kutangazwa kuingoza mexico

Jose Manuel De La Torre anatazamiwa kutangazwa hii leo jumatatu kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Mexico baada kuondoshwa kwa mshangao wa wengi baadhi ya majina makubwa yaliyokuwa yakitajwa kupewa nafasi hiyo huko nyuma.

Victor Manuel Vucetich kocha wa klabu ya Monterrey Rayados ya Mexico alikuwa na nafasi ya kutajwa kuingoza Mexico lakini jina lake limeondoshwa jumamosi kwa kile kilicho elezwa kuwa ni sababu binafsi.

Kura ilipigwa na wamiliki wa vilabu mbalimbali vya Mexico na kuamua kumtaka De La Torre kabla ya kuleta mvutano mkubwa juu ya majina kadhaa ambayo yalikatwa kwasababu mbalimbali.

Timu ya taifa ya Mexico imekuwa katika mazingira kutatanisha hususani baada ya kufungwa dhidi ya Argentina katika mchezo wa mzunguko wa pili wa michuano ya kombe la dunia na wasiwasi ukaanza kujitokeza juu ya uwezo wa kocha.

Kipigo hicho kilifuatiwa na kujiuzulu kwa Javier Aguirre na makocha wengine wawili wa muda Enrique Meza na Efrain Flores na kusababisha hali ya sintofahamu ndani ya timu ya taifa ya Mexico.

Kundi la wachezaji 11 players akiwemo nahodha wa kombe la dunia Rafael Marquez walitishia kumgomea mkurugenzi wa timu Nestor De La Torre juu ya maamuzi yake ya kuwapiga fine wachezaji hao kufuatia kitendo chao cha kufanya party huko Monterrey baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Colombia mwezi September.

Wachezaji wawili Carlos Vela wa Arsenal na Efrain Juarez wa Celtic walijikuta wakikumbwa na adhabu ya kusimamishwa kwa miezi sita kuichezea timu hiyo baada ya tukio hilo lakini hata hivyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Venezuela mapema mwezi huu wachezaji hao wakajumuishwa lakini Nestor De La Torre akaamua kujiuzulu nafasi yake masaa machache kabla ya mchezo.

No comments:

Post a Comment