KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, October 4, 2010

KIUNGO WA NEWCASTLE BEN ARFA AVUNJIKA MGUU Kiungo wa Newcastle United Hatem Ben Arfa amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuvunjika mfupa aina ya tibia and fibula katika mchezo dhidi ya Manchester City mchezo ambao City walimaliza kwa ushindi wa mabao 2-1 klabu yakwe toka Tyneside imethibtisha.
Ben Arfa mwenye umri wa miaka 23 alidondoka baada ya kukumbana na kigingi cha Nigel De Jong dakika nne tu ya mchezo kabla ya kuchukuliwa na kukimbizwa hospitali akiwa kwenye machela.
Kwa mjibu wa mtandao wa klabu umethibitisha kuwa amekutwa na makeraha na anataraji kufanyiwa vipimo jumatatu

KOCHA ROY HODSON ANG'AKA JUU YA MFUMO WAKE USIO NA TIJA LIVERPOOL




Hodgson 'insulted' by questioning
Roy Hodgson amejipanga kutafuta namna ya kujitetea katika umeneja wake ambapo tayari Liverpool ikiwa karti kuti kavu katika msimamo wa ligi kuu ya uingereza.
Roy Hodgson anaonekana kuchukizwa na maswali yanayo husiana na mfumo wale wa kiuchezaji
Hodgson amekuwa katika wakati mgumu Anfield baada ya matokeo mbaya na uchezaji mbovu wa timu hiyo katika michezo ya kigi na hata michezo ya Carling Cup ambapo walikubali kuaaga mbele michuano hiyo toka kwa timu ndogo ya League Two ya Northampton
Hata hivyo Hodgson aliye wahi kufanya vizuri katika nchi za Sweden na Denmark na hata kufika fainali mara mbili za viabu Europa bado ana amini kuwa hakuna linalo stahili kuzunguzwa juu yake kwa sasa licha ya matokeo hayo mabovu.
Alipoulizwa kuhusu mfumo wake wa kiuchezaji kushindwa anasema
"haamini hilo na kumuuliza mwandishi aliye uliza swali hilo anaa maanisha nini juu ya swali lake na kumuhoji katika kipindi cha miaka 35 amepitia vilabu vingapi na hilo lionekane leo?
"What do you mean do my methods translate? They have translated from Halmstads to Malmo to Orebo to Neuchatel Xamax to the Swiss national team, so I find the question insulting.
"kuzungumzia hilo, kwasababu nimekuwa nikihama kutoka klabu moja kwenda klabu nyingine ni kwasababu ya mfumo huo na nimekuwa nikifanya hivyo kwa miaka 35 wewe unasemaje habari ya mfumo nimekuwa ni kocha mwenye heshima.
"Experience is an important quality for any manager.


BLUES YAIKANDAMIZA GUNNERS ILHALI REDS SIKIO LA KUFA

Chelsea imejiweka katika mazingira mazuri ya kutetea taji lake ubingwa wa ligi kuu ya kandanda nchini Uingereza baada ya kupata ushindi safi wa mabao 2-0 mbele ya washika bunduki Arsenal 2-0 mchezo ambao umepigwa katika dimba la Stamford Bridge.
Didier Drogba ambaye amekuwa mwiba mara zote kwa Arsenal timu hizo zinzpo kutana katika miaka ya hivi karibuni ndiye aliyekuwa wa kwanza kufungua bao la uongozi karibu na kuelekea mapimziko katika kipindi ambacho kilikuwa ni kigumu na kuupeleka mpira nyuma ya Lukasz Fabianski dakika ya 39 ya mchezo.
Bao la pili la washindi hao liliwekwa kimiani na mlinzi Alex kunako dakika ya 85 baada ya kupiga mpira wa free-kick toka upande wa kona .


Mchezo mwingine pressure imezidi kupanda kwa kocha wa Liverpool Roy Hodgson baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 toka kwa Blackpool tena wakiwa nyumbani Anfield. Dalili mbaya kwa Liverpool zilionekana mapema kufuatia mshambuliaji wake hatari Fernando Torres kukutana na maumivu ya mteke katika dakika ya tisa ya mchezo na kulazimika kutoka nje na dakika chache baadaye Sotirios Kyrgiakos akashuhudia mpira wake wa kichwa ukiokolewa katika mstari wa goli na mambo kuendelea kuwa mabay zaidi kwa upande wa Liverpool pale Charlie Adam alipo kandamiza bao la kuongoza kwa njia ya mkwaju wa penati baada ya Glen Johnson kumuweka chini Luke Varney katika eneo la hatari. Varney baadaye akazidi kuikandamiza Liverpool kwa bao la pili la Blackpool muda mfupi kabla ya mapumziko.
Liverpool walianza kupumua mapema katika kipindi cha pili kwa bao la Kyrgiakos bada ya kupokea mpira free-kick wa Steven Gerrard hata hivyo vijana wa Ian Holloway walijikuta katika furaha baada ya kushuhudia dakika tisini zikimalizika kwa ushindi huo wa mabao hayo 2-1 ugenini Anfiled.

Mchezo mwingine Adam Johnson akitokea katika benchi amefanikisha ushindi wa mabao 2-1 wa Manchester City na kuwaweka katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi baada ya kuichapa Newcastle United mabao 2-1 nyumbani Eastlands katika dimba la City of Manchester . Mabao ya washindi yakifungwa na Crlos Tevez kwa njia ya mkwaju wa penati kunako dakika ya 18 ya mchezo



kabla ya Newcastle kusawazisha kupitia kwa Jonas Gutierrez kunako dakika ya 24 na baadaye kunako dakika ya 75 ya mchezo Adam Johnson kuihakikishia City points zote tatu muhimu.
Matokeo hayo yanaiweka City nyuma ya vinara Chelsea wenye points 18 na City wakikusanya jumla ya points 14.

No comments:

Post a Comment