KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, July 19, 2011

Bayer Leverkusen yathibitisha mazungumzo na Juventus kwa ajili ya Arturo Vidal

Mkurugenzi mtendaji wa w a klabu ya Bayer Leverkusen ya nchini ujerumani Wolfgang Holzhauser amesema klabu yake ipo katika mazungumzo na Juventus ya italia juu ya mpango wa uhamisho wa nyota Arturo Vidal.
Imethibitika mapema jinsi ambavyo klabu hiyo ya italia kutaka kukutana na wakala wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 Fernando Felicevich mwishoni mwa juma hili.
Vidal ambaye timu yake ya taifa ya Chile ilitolewa mapema katika michuano ya Copa America amekuwa akihusishwa na kutaka kuondoka katika ligi kuu ya kandanda nchini ujerumani maarufu kama Bundesliga club.
Holzhauser sasa amethibitisha juu ya mazungumzo na kibibi kizee hicho cha Turin.

Anakaririwa na mtandao wa Tuttomercatoweb.com amesema
"naweza kuthibitisha kuwa tuko katika mazungumzo na Juventus kuhusu Vidal,"
"sasa inaonekana wazi kuwa hataweza kuch
eza
katika ligi ya

ujerumani msimu ujao."

Bayern Munich pia imeonyesha nia ya kumnasa Vidal, lakini klabu yake ya sasa haiku tayari kumuuza kwa wapinzani wao wakubwa katika Bundesliga.
Mchezaji mwenyewe huko nyuma alitaka zaidi kujiunga na Bayern, lakini baadaye akabadilisha nia na kutaka sasa kujiunga na ligi ya nchini Italia.
Nyota huyo wa zamani wa Colo-Colo mkataba wake wa sasa na Leverkusen unatarajiwa kumalizika 2012,lakini inaonekana wazi kuwa Juventus italazimika kulipa pauni milioni €15 kufidia huduma mbalimbali
.

No comments:

Post a Comment