Arsenal yatoa wiki mbili kwa Barcelona kukamilisha ombi lao la offer ya pauni milioni €45 kumnasa Cesc Fabregas
Arsenal imearifiwa kutoa majuma mawili kwa Barcelona kukamilisha utoaji kwa kitita cha pauni milioni €45 kwa ajili ya kiungo Cesc Fabregas.
Kiungo huyo mwenye umri wa 24 aliondoka nyumbani Catalan mwaka 2003 na kujiunga na Gunners ambako amekamilisha kucheza jumla ya michezo 300 akiwa na klabu hiyo .
Na katika misimu ya hivi karibuni amekuwa akionyesha nia ya kutaka kurejea katika klabu yake hiyo ya zamani Barca wakati wowote katika maisha yake ya kucheza soka.

Gazeti la The Sun limearifu kuwa klabu hiyo toka London ya kaskazini imeweka wazi kwa kigogo hicho cha Hispania wanalo la kuchagua ama kufikia makubaliano hayo ndani ya wiki mbili au kuandika kumkosa London outfit have Fabregas.
Mambingwa hao wa kandanda barani ulaya wamekuwa wakihusishwa na kumtaka kiungo huyo lakini hata hivyo Rais wa klabu hiyo Hispania Sandro Rosell huko nyuma alikaririwa akisema klabu yake ina bajeti ya pauni €46 kwa ajili ya usajili mzima wa klabu katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi.
Katika hatua nyingine gazeti la Daily Mail linaripoti kuwa kiungo huyo atakutana na meneja wake wa sasa Arsene Wenger kuweka mkazo juu ya mpango huo wa uhamisho wake.
Inaaminika kuwa bosi wa Gunners ameahirisha mpango wa kumuondoa kiungo huyo lakini pia inaarifiwa katika jitihada zake amefanikiwa kumbakisha ndani ya Emirate mshambuliaji wake Samir Nasri.
No comments:
Post a Comment