Chama cha kandanda nchini Brazil kimesema kocha wake Mano Menezes atasalia licha ya kuondoshwa katika Copa America Kocha wa timu ya taifa ya Brazil Mano Menezes hatapoteza kibarua chake cha kuifundisha timu ya taifa ya nchi hiyo licha ya timu ya taifa ya Brazil kuondoshwa katika michuano ya Copa America na atakuw a akiendelea kukonoa kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya maandalizi ya fainali ya kombe la dunia mwaka 2014 hizo zikiwa ni taarifa toka chama cha kandanda cha Brazil zilizo toka hii leo.
Kumekuwepo na maswali mengi juu ya hatma ya baadaye ya kocha huyo ambaye pia ni kocha wa zamani w a timu ya Corinthians kufuatia kuvurunda katika Copa America katika hatua ya robo fainali.
Timu ya taifa ya Brazil maarufu kama Selecao imeondoshwa na Paraguay katika mchezo wa robo fainali iliyofikia mpaka katika hatua ya mikwaju ya penati na hivyo kuharibu mwenendo mzuri wa mfululizo wa kutwa mataji mawili ya michuano hiyo katika fainali mbili zilizopita barani Amerika ya kusini.
Brazil katika mchezo huo ilikwenda sare ya bila mabao mpaka kukamilika kwa muda wa nyongeza na kujikuta wakikosa penati nne na washindi Paraguay kupata penati mbili za ushindi.
Katika taarifa iliyotolewa nah ii leo na shirikisho la kandanda nchini Brazil CBF imesema Menezes alikuwa ni mtu wa kuwapeleka mbele zaidi na kwamba hatma yake bado ipo palepale kuiongoza timu ya taifa .
Taarifa imesema
"hakuna haja ya kulalamikia tena juu ya kuondolewa katika Copa America,ambapo imetokezea katika hali kama hiyo kwa maana ya penati hii leo hususani ni baada ya miaka 17 ya mafanikio ya kupata mataji manne duniani.
"kwa sababu hiyo Rais Ricardo Teixeira amempigia simu Mano Menezes mwisho wa mchezo na kumthibitishia mpango wa kujenga kikosi cha timu ya taifa unaendelea na kwamba aendelee na mipango yake aliyo anza nayo kwa ajili ya kombe la dunia 2014."

No comments:
Post a Comment