Esperance na Cotonsport waanza vizuri ligi ya mabingwa
Esperance ya Tunisia yapata sare ya bao 1-1 dhidi ya Mouloudia Alger ya Algeria katika kundi B.
Cotonsport iliyokuwa na wachezaji kumi uwanjani yapata sare ya 0-0 ugenini dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco katika kundi A.
Timu ya Cotonsport ya Cameroon imefanikiwa kupata matokeo hayo licha ya kuwakosa wachezaji wake watatu muhimu ambao wamesimamishwa.
Kiungo Oussama Darragi ndiye aliyekuwa wa kwanza kuipa Esperance bao la mapema dhidi ya mambingwa wa zamani wa taji hilo huku mlinzi mzoefu Mohamed Meghirbi akisawazisha dakika tisa baadaye.
Hata hivyo Cotonsport waliweza kuziba mapengo ya wachezaji wao nyota na hata baada ya mwenzao mmoja kupewa kadi nyekundu zikiwa zimesalia dakika 13 kabla ya mchezo kumalizika walilazisha sare hiyo.
Esperance ambayo imefanikiwa kushinda michuano yoye ya Pan-African isipokuwa “Confederation Cup” ilikuwa na matumaini ya kufika nusu fainali toka kundi B sambamba na Al Ahly ya Misri ambao walikuwa dimbani dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco jumapili hii.
No comments:
Post a Comment